Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yajue mambo matatu yanayomsononesha ‘Bwege’

Mbunge Mstaafu wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara maarufu ‘Bwege’.

Muktasari:

  • Mbunge Mstaafu wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara maarufu ‘Bwege’ ametaja mambo matatu yanayomuumiza tokea astaafu Ubunge mwaka 2020.

Lindi. Mbunge Mstaafu wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara maarufu ‘Bwege’ ametaja mambo matatu yanayomuumiza tokea astaafu Ubunge mwaka 2020.

Jambo la kwanza ni uwanja wa mpira uliopo Kilwa Masoko ambao alikuwa akichangia asilimia kumi ya fedha za jimbo kila zilipoingia kwa ajili ya kuuboresha, ambapo kwa sasa unamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi, (CCM).
Amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Pombe Magufuri alipoagiza mali za CCM ziorodheshwe kwa bahati mbaya uwanja huo pia uliorodheshwa.
“Hawakuwa na hati yoyote, mpaka mimi naacha Ubunge hawakuonyesha hati hata siku moja, hili jambo linaniuma sana kwamba uwanja wa Halmashauri wanataka kuuchukua CCM” amesema Bwege.
Jambo la pili amesema ni kitendo cha ofisi za halmashuri ya wilaya ya Kilwa kujengwa eneo la Lingaula kilometa 32 kutoka yalipo makao makuu ya halmashauri.
“Tulidai sana kwanza udongo wa kule ni mfinyanzi ujenzi wake gharama, pili nyumba zaidi ya kumi za wakuu wa idara zipo huku Masoko, gharama itakuwa kubwa ya usafiri na hoja nyingine, halmashauri zinaundwa kwa ajili ya kuwa karibu na wananchi kule hakuna nyumba wala kitu chochote hii ni kinyume na mwongozi wa halamshauri” amesema Bwege.
“Hata ukiangalia taasisi na mamlaka mbali mbali za nchi kama TRA, benki, Maji, Bandari kila kitu kipo Masoko leo Halmashauri ikajengwe huko sawa sawa na kichwa kina vitu vyote lakini macho yawe chini ya unyayo”.
Bwege amesema ACT Wazalendo watafanya maandamano wilayani humo kulaani mambo hayo mawili yanayomuumiza.  
Jambo la tatu ni mradi wa maji kutoka Mavuji kuja Kilwa kivinje na Masoko ambao aliishawishi serikali kipindi hicho na mradi ukakubalika na kupatikana wafadhili kutoka India, ameiomba serikali ya wilaya hiyo kuukamilisha ili kutatua tatizo kubwa la maji katika miji ya Masoko na Kivinje.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai amesema amekuta ujenzi ukiendelea wa ofisi za Halmashauri na kuelezwa kuwa mchakato ulianza awamu ya nne ambapo Halmashauri iliongozwa na upinzani kutokana na ufinyu wa eneo huku Masoko.
“ACT, CUF na CHADEMA wao ndio walipendekeza leo mawazo yao wanayakataa, ni mchezo wa siasa tu Masoko hapa unapoingia ni kama kwenye chupa ya soda kukifungwa huwezi kutoka lakini Lingaula unaweza kutokea njia ya Dar es Salaam, Lindi, Liwale hata kiulinzi ni shida,” amesema Mkuu huyo.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Aston Ngwilangwa amesema kuwa kiwanja cha michezo ni mali ya CCM.
“Zamani ulikuwa unasimamiwa na halmashauri, baadaye CCM ilianza kuhakiki mali zao walipofika moja ya vitu ambavyo walikuta Halmashauri inasimamia lakini sio mali zake ni uwanja kwa hivyo ikauchukua” amesema Ngwilangwa.