Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuu Ethiopia akutana na wapinzani

Muktasari:

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa, Leta alimwambia mwanahabari kwamba matokeo ya mazungumzo yetu yamewezesha ODF kushiriki siasa za Ethiopia.

 


Addis Ababa, Ethiopia. Waziri Mkuu Dk Abiy Ahmed amekutana na wawakilishi wa chama cha upinzani kilichokuwa kinafanya shughuli za uhamishoni cha Oromo Democratic Front (ODF) baada ya chama hicho kukubali kushiriki mjadala wa siasa za Ethiopia kwa amani.

Katika taarifa yake ya Mei 13, 2018 ODF ilithibitisha kwamba ilifikia makubaliano na Serikali baada ya kufanya mazungumzo katika eneo ambalo halikuwekwa wazi warudi nyumbani washiriki katika mchakato wa kidemokrasia.

Viongozi wa ODF wakiongozwa na Mwenyekiti wa Front Lencho Leta waliwasili jijini Jumatano iliyopita.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa, Leta alimwambia mwanahabari kwamba matokeo ya mazungumzo yetu yamewezesha ODF kushiriki siasa za Ethiopia.

“Kwa kuzingatia masharti na namna mazungumzo na Serikali yatakavyokuwa, ODF itaamua kufanyia shughuli zake za kisiasa katika ardhi ya Ethiopia na kuanzisha muungano na vyama vingine vya siasa,” alisema Leta.

Shirika la Utangazaji la Serikali la Fana BC liliripoti kwamba pande zote mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja ili kujenga umoja wa taifa na kuimarisha mchakato wa kidemokrasia.

Leta aliongeza kwamba chama chake kimekubali kurudi nchini baada ya kuridhishwa na mchakato wa mageuzi ya demokrasia yanayoendelea.