Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuu apokea ripoti ya moto Soko la Kariakoo

Muktasari:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi wa tukio la moto uliotokea katika soko la kimataifa la Kariakoo Julai 10, 2021 jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi wa tukio la moto uliotokea katika soko la kimataifa la Kariakoo Julai 10, 2021 jijini Dar es salaam.

Majaliwa amepokea taarifa hiyo leo Jumanne Julai 27, 2021 kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hayo, CP Liberatus Sabas na kuahidi kuwa Serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolkewa na kamati hiyo.

Akizungumza baada ya kuipokea taarifa hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Majaliwa amewashukuru na amewapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa weledi mkubwa.

Majaliwa amesema ataifikisha taarifa hiyo kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwani tukio hilo limewagusa watu ndani na nje ya nchi.

“Naahidi mbele yako mwenyekiti kuwa Serikali nimeridhishwa na taarifa mliyo nikabidhi leo na mapendekezo yote mliyoyatoa yatazingatiwa.

Jumapili Julai 11, 2021 Majaliwa alipotembelea na kukagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa kudhibiti moto katika soko la kimataifa la Kariakoo alitangaza kamati ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto huo.

Julai 21, 2021 Majaliwa aliongeza siku saba kwa kamati aliyoiunda kuchunguza kuungua kwa soko la Kariakoo hadi Julai 25, mwaka huu.