Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mchengerwa aagiza TFS kuongeza kasi upandaji miti

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa akiangalia moja ya  mashine zinaonyeshwa na kampuni ya FarmBase Limited kwenye maonyesho ya Nanenane Kanda ya mashariki katika viwanja vya Julius Nyerere Morogoro. Picha na Lilian Lucas.

Muktasari:

  • Misitu ni uhai na mategemeo ya wizara ni kwenda sambamba na kinachopandwa huku wakitakiwa kuangalia utaratibu wa kudhibiti ubadhilifu wa misitu.

Morogoro. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa ameagiza wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kuongeza kwa kasi upandaji wa miti, kutengeneza mashamba mapya na kuyalinda ya mashamba ya zamani ili kasi hiyo iwe yenye tija.

Mchengerwa amesema hayo alipotembelea Maonyesho ya NaneNane Kanda ya Mashariki katika Viwanja vya Julius Nyerere Morogoro.

Ametoa maagizo hayo akiwa katika Banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Amesema misitu ni uhai na mategemeo yake yaendane sambamba na kinachopandwa na waangalie utaratibu wa kudhibiti ubadhilifu wa misitu.

Amesema Kama wanatoa kibali cha mtu kwenda kuvuna waende wakasimamie na kwamba makontena yanayopakia mzigo yahakikiwe, kukaguliwa kwani kuna upotevu mkubwa wa fedha zinazotokana na misitu.

"Tumezuia vibali vyote vya mkaa kwa watu wanaotumi pikipiki kwa sababu ya usababishaji wa ajali anayetakiwa ni yule ambaye ana usafiri wa miguu mitatu au mine," amesema.

Aidha ameitaka TFS kudhibiti uvunaji mkaa kwa kuanzia kwenye mapori na si kuwakamata barabara wale wabeba mkaa jambo ambalo limekuwa likisababisha ajali kwa wakati mwingine.

"TFS sitegemei kuona TFS  mnakamata watu barabarani, ukamataji uishie porini sababu barabarani kunakuwa na vurugu nyingi, "amesema.

Wakati huohuo Waziri Mchengerwa ameziagiza taasisi zote zilizopo chini ya wizara yake kuendelea kutangaza utalii na kuongeza mapato katika pato la Taifa ambapo ameeleza kuwa mpaka ifikapo 2025 wizara imelenga kuchangia zaidi ya Sh10 trilioni kutoka Sh7 trilioni ya sasa.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema maendeleo ya kiuchumi na Kijamii kwa Kanda ya mashariki yanaendana sambamba na utekelezaji ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kamanda wa Kanda ya Mashariki TFS, Mathew Ntilicha amesema wakala huo unaendelea kusimamia mianya yote yenye kupitisha ubadhilifu katika mapori ya misitu na kwamba wameendelea kuitumia Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Tofori) kutokana na tafiti wanazofanya ili kuelimisha wananchi juu ya utunzaji wa misitu na mazingira.