Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazindua mwonekano mpya bajaj miguu mitatu

Muktasari:

Kampuni ya kutengeneza pikipiki za magurudumu matatu ya Bajaj Auto kwa kushirikiana na kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (METL) Group imezindua pikipiki mpya ya matairi matatu yenye uwezo wa kubeba watu saba.

Dar es Salaam. Kampuni ya kutengeneza pikipiki za magurudumu matatu ya Bajaj Auto kwa kushirikiana na kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (METL) Group imezindua pikipiki mpya ya matairi matatu yenye uwezo wa kubeba watu saba.

Pikipiki ya aina hiyo yenye injini ya 236cc ndiyo ya kwanza kuingia katika soko la Tanzania. Kampuni ya METL Group pekee ndiyo itasambaza pikipiki hizo za magurudumu matatu zenye namba RE250 ambazo sasa zinaingia nchini na kusambazwa kwa wafanyabiashara.

Mkurugenzi wa masoko wa METL, Fatema Dewji alisema: "kampuni kupitia bidhaa zake bora na utoaji wa huduma na mipango ya ustawi, tutaanzisha ushirikiano wa muda mrefu na mfumo wa ikolojia na wateja kote Tanzania kama tulivyofanya kwenye bodaboda.

"Kupitia washirika hawa tunalenga kutoa fursa za ajira kwa Watanzania milioni 5  za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika kipindi cha miaka 5 ijayo,” alisema mkurugenzi huyo.

Akizungumzia hafla hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bajaj wa METL, Indrabhuwan Kumar Singh alisema: “Tanzania ni miongoni mwa masoko muhimu ya pikipiki za matairi matatu duniani na tumetengeneza pikipiki hii maalum kwa ajili ya Tanzania. Kwa mfano, kila mara tumehisi kwamba mpanda Bajaj nchini Tanzania anahitaji injini kubwa na yenye nguvu zaidi kwa sababu ya hali ngumu ya barabara.”

"Tunafuraha kuzindua RE250 kwa waendesha bajaj wetu wa Tanzania na tunaamini kuwa itasaidia waendeshaji na wamiliki kufanikiwa maishani mwao."

Wafanyabiashara walioalikwa kwenye hafla ya uzinduzi huo walipongeza ubunifu huo ambalo walisema soko "linauhitaji sana."

Kwa kupitia pikipiki hiyo mpya ya magurudumu matatu ambayo inapatikana kupitia wafanyabiashara wa ndani, kampuni hiyo  inatarajia kupata nafasi kubwa katika soko la Tanzania.