Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazawa watakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji

Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kanda ya Kaskazini, Daud Riganda

Muktasari:

Watanzania wametakiwa kujitokeza kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo nchini na kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, kilimo na utalii ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Moshi. Watanzania wametakiwa kujitokeza kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo nchini na kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, kilimo na utalii ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Rai hiyo imetolewa na meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kanda ya Kaskazini, Daud Riganda wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshikuhusiana na hali ya uwekezaji katika kipindi cha mwaka mmoja, ambapo amesema hali kwa sasa inaridhisha.

Amesema katika kipindi cha mwezi Machi 2021 hadi Machi 2022, jumla ya miradi 31 ya uwekezaji yenye thamani ya dola za Kimarekani 424.84 milioni, imeandikishwa katika kanda ya kaskazini huku kwa asilimia kubwa wawekezaji wakiwa ni kutoka nje ya nchi.

Amesema katika miradi hiyo, miradi 13 ni miradi ambayo wawekezaji wake wanatoka nje ya nchi, miradi 10 ikiwa ya ubia kati ya Watanzania na wawekezaji kutoka nje, huku miradi 8 ikiwa ya wawekezaji Watanzania.

"Hali ya uwekezaji Kanda ya Kaskazini inaridhisha, katika kipindi cha mwaka mmoja jumla ya miradi 31 iliandikishwa na miradi hii inatarajiwa kuwa na mtaji wa thamani ya Dola za Kimarekani 424.84 milioni na itatengeneza ajira 6,595 na kati ya miradi hiyo, miradi 13 ni miradi ambayo wawekezaji wake wanatoka nje ya nchi, " amesema Riganda.

Ameongeza kuwa "Natoa rai kwa Watanzania, kwa kuwa hizi rasilimali ni za kwetu ni vyema wakatumia fursa za kilimo, viwanda, utalii, usafirishaji, nishati, madini, mawasiliano, na nyingine tulizojaliwa kwa wingi kuwekeza, badala ya kutegemea wageni kutoka nje ya nchi pekee".


Akizungumzia faida za Royal Tour katika uwekezaji, Riganda amesema wanayo matarajio makubwa ya kuongeza idadi ya wawekezaji kupitia filamu hiyo, ambayo imeonyesha rasilimali mbalimbali zilizopo nchini pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo.

"Kiuwekezaji tunayo matarajio makubwa maana tunaamini itaongeza idadi ya wawekezaji hapa nchini, lakini pia itachochea ongezeko la watalii na taarifa tulizo nazo ni kwamba tayari mahoteli yameanza kujaa, hivyo itaamsha uwekezaji kupitia hoteli na makampuni ya utalii"

Naibu waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema filamu hiyo imeipaisha nchi na kuionyesha dunia kuwa Tanzania ni moja ya nchi yenye vivutio vingi vinavyotikisa.

Dk Mollel ambaye ni mbunge wa Jimbo la Siha amesema wao kama wabunge wanapaswa kusimamia mifumo ambayo inasaidia wawekezaji wanaowekeza kwenye sekta ya utalii na kwingine, ili waweze kuwekeza kirahisi na kutengeneza faida pamoja na kuitangaza zaidi nchi kimataifa.

"Nitoe wito kwa wananchi kutambua kuwa kuna fursa nyingi za uwekezaji, wajitokeze kuwekeza katika utalii na hata katika nyanja mbalimbali hapa nchini, hatua ambayo itachochea ukuaji wa uchumi".