Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wavuvi waomba Serikali kudhibiti uvamizi Ziwa Victoria

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Hamad Masauni akizungumza na baadhi ya wavuvi katika mwalo wa Sota wilayani Rorya. Picha na Beldina Nyakeke 

Muktasari:

Kwa mujibu wa mgawo wa Kimataifa, Tanzania inamiliki sehemu kubwa ya Ziwa Victoria ikiwa na asilimia 51 ikifuatiwa na Uganda inayomiliki asilimia 43 huku Kenya ikiwa na asilimia sita ya ziwa lote.

Rorya. Wavuvi wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara wameiomba Serikali kuingilia kati na kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi Ziwa Victoria ikiwemo kudhibiti  vitendo vya uvamizi vinavyodhaniwa kufanywa na wavuvi kutoka nchi za jirani.

Wakitoa malalamiko yao kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni aliyefanya ziara katika mwalo wa Sota wilayani Rorya Aprili 8, 2023, baadhi ya wavuvi wamedai kuvamiwa na wavuvi wenzao kisha kuporwa mali zao hali ambayo imekuwa ikiwafanya kutofanya kazi zao kwa tija.

“Matukio ya uvamizi yamekuwa mengi sana hapa hata jana(Aprili 7) kuna tukio limetokea na matukio haya yamekuwa yakitusababishia hasara tunaporwa mali zetu ikiwemo mashine, samaki, boti na hata wengine kupoteza maisha,”amesema Ramadhan Ng'wina mmoja wa wavuvi wa mwalo wa Sota

Ng'wina amesema pamoja na mambo mengine hali hiyo inasababishwa na kutokuwepo kwa doria za uhakika tofauti na askari wa nchi za jirani wanavyofanya.

“Serikali imekisahau kituo cha polisi wana maji cha Sota kwasababu hakina boti wala askari wa kutosha sasa wale wavamizi wanatumia fursa hiyo kutuvamia hadi huku kwenye maji yetu na kufanya uhalifu,” amesema mvuvi mwingine, Omary Hassan

Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amesema vitendo hivyo vya uvamizi ziwani vinaendelea kushamiri licha ya jitihada zinazofanywa na serikali wilayani humo kukabiliana navyo.

Chikoka amesema Ziwa Victoria lina thamani kubwa kwa maisha ya  wakazi wa wilaya hiyo kwani linagusa moja kwa moja  maisha yao hivyo uwepo wa vitendo vya uhalifu ziwani humo zinarudisha nyuma juhudi za Serikali kupambana na umasikini kupitia rasilimali hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Hamad Masauni amesema jukumu la Serikali ni kuhakikisha wavuvi wanatekeleza majukumu yao kwa usalama na amani.

Amewaambia wavuvi hao Serikali imepanga kushughulikia jambo hilo kwa mipango ya muda mrefu na muda mfupi ili kuhakikisha kuwa changamoto hiyo inapata suluhisho la kudumu 

“Kwanza niwape  pole kwa haya yanayotokea na Serikali haiwezi kukaa kimya wakati watu wake wanaumia, sasa kabla ya mambo mengine naahidi kuleta boti hapa kwaajili ya kuimarisha doria,”amesema

Amesema kutokana na uchakavu wa kituo cha polisi cha wana maji Sota Serikali inakusudia kujenga kituo hicho ili kiwe cha kisasa na kuongeza idadi ya maaskari sambamba na vifaa kwaajili ya doria itakayosaidia kudhibiti vitendo hivyo na hatimaye wavuvi hao kufanya kazi zao kwa amani na utulivu.

“Nikiri tu kuwa kituo chetu kimechoka na ni cha zamani, miundombinu yake ya zamani, haikidhi mahitaji pia kinachangia kushusha ari ya utendaji kazi. Niwaahidi kuwa Serikali inakwenda kushughulikia changamoto hizi kwani moja ya majukumu ya Serikali ni usalama wa wananchi wake muda wote,”amesema