Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto wawili wafariki banda la kuku likishika moto

Muktasari:

Watoto hao wawili wamefariki baada moto kulipuka katika banda la kuku walimokuwa wakicheza, huku mtoto mwingine akijeruhiwa na moto huo.

Ludewa. Watoto wawili Meshack Ndimbwa (6) na Agrey Mgimba (2) wamefariki dunia na mmoja kulazwa baada ya kuungua na moto wakiwa wanacheza kwenye banda la kuku kijiji cha Lugarawa Wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Akizungumza na Mwananchi leo Oktoba 31, Mwenyekiti wa kijiji cha Lugarawa amesema tukio lilitokea Oktoba 29 majira ya asubuhi.

“Tukio hili lilitokea Jumamosi majira ya asubuhi, ambapo watoto hao walifariki wakati wakicheza ndani ya banda la kuku,” amesema Kayombo


Ameongeza kuwa chanzo cha banda kuungua ni moto uliopulizwa na upepo kutoka kwa jirani aliyekuwa anachoma mabua.

“Kuna kijana alikuwa anachoma mabua nyumbani kwake, nyumba yake inapakana na nyumba yenye vibanda vya kuku na nguruwe ambapo watoto wale walikuwa wakicheza, yeye baada ya kuchoma ule moto na kuona umetulia akaondoka.

“Ule moto ukapulizwa na upepo ukashika vile vibanda vya nyasi, sasa walipo kuwa ndani na kuona moto unakuja mtoto mmoja mkubwa alitoka na kukimbia wawili wakabaki ndani,

“Baadaye alirudi ili kuwaokoa wenzake, kwa bahati nzuri pale jiarani palikuwa na fundi anapaua nyumba baada ya kuona yule anarudi akaruka kwenda kumuokoa akamkamata lakini alikuwa amesha ungua,” amesema Kayombo

Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya St. John’s Lugarawa, Dk Camilo Msigwa, amesema alipokea miili ya watoto wawili wakiwa wamefariki huku mmoja akilazwa kutokana na majeraha ya moto huo.

“Majeruhi anaendelea na matibabu hali yake sio mbaya sana, kwani ameungua sehemu za kichwa, kifua na mikono.

“Wauguzi wanaendele kumpatia huduma lakini wenzake walifariki hapo hapo,” amesema Dk Msigwa.

Ameongeza kuwa marehemu waliungua vibaya na kulazimu kuzikwa siku hiyo hiyo.

“Marehemu waliungua vibaya kiasi kwamba yule mdogo fuvu lilikuwa karibu limeteketea mpaka vitu vya ndani vinaonekana na utumbo umetoka nje.

“Tukawashauri wasiwahifadhi wakazikwa siku hiyo hiyo jioni,” amesema Dk Msigwa 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.