Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu ndio uhaini anaoshtakiwa nao Lissu 

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu (57) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, akikabiliwa na kesi mbili tofauti za jinai zenye mashtaka tofauti, likiwemo la uhaini.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu (57) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, akikabiliwa na kesi mbili tofauti za jinai zenye mashtaka tofauti, likiwemo la uhaini.

Lissu amepandishwa kizimbani leo Alhamisi, Aprili 10, 2025, jioni na kusomewa mashtaka hayo na mawakili wawili mbele ya mahakamu wawili tofauti.

Katika kesi ya kwanza, Lissu amesomewa shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawishi, Franco Kiswaga, akidaiwa kutenda kosa hilo Aprili 3, 2025 ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Akimsomea shtaka hilo Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga amesema katika tarehe hiyo Lissu, raia wa Tanzania kwa nia ya uchochezi alishawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Katuga amesema kwa kuthibitisha nia hiyo ya uasi kwa kushinikiza kiongozi mkuu wa Serikali ya Tanzania akitamka na kuandika maneno yafuatayo:

"Wakisema msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli..., kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, hivyo ndivyo namna ya kupata mabadiliko..., kwa hiyo tunaenda kukinukisha..., sana sana huu uchaguzi tutaenda kuuvuruga kwelikweli..., tunaenda kukinukisha vibaya sana..."

Kwa mujibu wa kifungu hicho cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, mtu yeyote atakayepatikana na hatia atawajibika kwa adhabu ya kifo.

Wakili Kaguta ameileza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Hakimu Kiswaga amesema shtaka linalomkabili ni la uhaini na halima dhamana na mshtakiwa hatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhaini.

Hata hivyo, kiongozi wa jopo la mawakili wa Lissu, Dk Rugemeleza Nshala amehoji sababu ya mteja wao kufikishwa mahakamani wakati upelelezi haujakamilika.

"Wao (upande wa mashtaka) wanajua sheria inawataka wanapomleta mtuhumiwa mahakamani upelelezi wake uwe umekamilika lakini kwa hili tunaona wanakiuka sheria," ameeleza Dk Nshala na kiuongeza:

"Ibara ya 14 ya Katiba ya Tanzania inatoa haki kulinda uhuru wa mtu. Kuweka kosa la uhaini na kumweka ndani ni kosa. Hivyo tunaomba mahakama ipange tarehe ya usikilizwaji wa awali. Na kama bado upelelezi utakuwa haujakamilika basi wamwachie hadi hapo upelelezi utakapokamilika,” amesema Dk Nshalla.

Wakili Katuga amepinga hoja hiyo akisema ingawa Dk Nshalla hakutaja kifungu cha sheria, lakini kifungu cha 131 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kinaainisha makosa makubwa ambayo mtuhumiwa anaweza kufikishwa mahakamani hata kabla ya upelelezi kukamilika.

Amesema kosa linalomkabili Lissu ni miongoni mwa makosa hayo makubwa ambayo hayahitaji upelelezi kukamilika.

Hakimu amekubaliana na hoja za upande wa mashtaka akisema sheria iko wazi na kwamba kwa mujibu wa vifungu vya 148 (5) cha CPA kosa hilo halina dhamana.

Hivyo, ameahiriaha kesi hiyo hadi Aprili 24 kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

Katika kesi ya pili, ambayo Lissu anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuchapisha mitandaoni taarifa za uongo, kinyume na Sheria ya Makosa ya Kimtandao namba 14 ya mwaka 2015, ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Geoffrey Mhini.

Mashtaka hayo yote matatu ni ya kuchapisha taarifa za uongo katika mtandao wa Youtube.

Akimsomea mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Lukosi Harrison amedai Lissu alitenda makosa hayo Aprili 3, 2025 jijini Dar es Salaa, kwa nia ya kulaghai umma.

Katika shtaka la kwanza, Wakili Harrison amenukuu maneno aliyoyachapisha Lissu kuwa:

"Uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 wagombea wa Chadema walienguliwa kwa maelekezo ya Rais, wakati akijua maneno hayo ni ya uongo na yanapotosha umma,” amedai.

Alipoulizwa na hakimu kama ni kweli au si kweli, Lissu amesema kuelezea ubovu wa uchaguzi si kosa, hivyo si kweli.

Shtaka la pili, anadaiwa siku hiyo alichapisha taarifa kuwa:

"Mapolisi wanatumika kuiba kura wakiwa na vibegi na kwamba maneno hayo ni ya uongo na ya kupotosha umma.

Hata hivyo, Lissu alipoulizwa amejibu kuwa kusema hivyo si kosa, hivyo si kweli.

Katika shtaka la tatu, anadaiwa siku hiyo hiyo alichapisha taarifa kuwa:

"Majaji ni Ma-CCM, hawawezi kutenda haki, wanapenda wapate teuzi na kuchaguliwa kuwa majaji wa Mahakama ya rufaa.

Alipoulizwa,na hakimu iwapo ni kweli ametenda kosa hilo,  Lissu alijibu kwa kusema majaji wanateuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na wanapenda kuteuliwa kuwa majaji wa rufaani, sio kosa hivyo sio kweli mheshimiwa.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka hayo na kuyakana, wakili Katuga alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na akaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea hoja za awali.

Hata hivyo, Dk Nshalla alidai mashtaka yanayomkabili Lissu yanadhaminika, hivyo anaomba mteja wake apewe masharti nafuu na kwamba wapo tayari kuendelea na hatua za hoja za awali hata Jumatatu ya wiki ijayo.

Hakukuwa na pingamizi ya dhamana bali Wakili katuba aliomba mahakama iweke masharti yatakayowezesha mshtakiwa kupatikana mahakamani atakapohitajika.

Hakimu Mhini alimtaka Lissu awe na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho cha Taifa (Nida) na barua ya serikali za mitaa, atakayesaini bondi ya Sh5 milioni.

Lissu amefanikiwa kudhaminiwa na shemeji yake aitwaye Rosemary Mushi, ambaye aliwasilisha barua kutoka Chadema, lakini Hakimu akamtaka awasilishe barua ya serikali za mitaa mahakamani hapo.

Hakimu Mhini ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 24, 2025 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa hoja za awali.

Hata hivyo, Lissu amepelekwa rumande kutokana na kesi ya uhaini ambayo haina dhamana.