Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KESI YA LISSU UPDATES: Arudishwa rumande

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Lissu amefikishwa mahakamani hapo leo Aprili 10, 2025 saa 10: 15 alasiri na kuwekwa kwenye mahabusu iliyopo mahakamani hapo.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.

XXXXXXXXXXXXX

KESI YA UHAINI: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka moja la uhaini.

Lissu amefikishwa mahakamani hapo leo Aprili 10, 2025 saa 10: 15, huku Wakili Nassoro Katuga akimsomea shitaka hilo.

Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dk Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.

XXXXX

KESI YA UHAINI HADI APRILI 24: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu imepigwa kalenda hadi Aprili 24, 2025.

Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka moja la uhaini leo saa 10.15 jioni,

Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dk Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.

XXXXXX

KESI YA TAARIFA ZA UONGO: Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amepandishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa kesi ya pili yenye mashitaka matatu ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa Youtube.

Awali leo Alhamisi Aprili 10, 2025 katika kesi nyingine alipandishwa kizimbani na kusomewa shitaka moja la uhaini, huku kesi hiyo ikipangwa kuendelea Aprili 24, 2025.

Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka moja la uhaini leo saa 10.15 jioni.
Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dk Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.

XXXXXXX

ARUDISHWA RUMANDE: Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, amerudishwa rumande baada ya kusomewa mashitaka yake leo Alhamisi Aprili 10, 2025.

Lissu amerudishwa rumande kutokana na shitaka la uhaini kutokuwa dhamana.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi