Watatu wajeruhiwa ajalini katika msafara wa Makamu wa Rais

Picha na Haiko Kimaro
Muktasari:
Ajali asubuhi leo mbele kidogo ya Nijiji cha Nanguruwe na majeruhi ambao ni dereva na wasaidizi wa makamu rais, wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Ligula.
Mtwara. Watu watatu wamejeruhiwa baada ya gari moja katika msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani uliokuwa unaelekea wilayani Tandahimba mkoani Mtwara kupinduka.
Ajali hiyo imetokea asubuhi leo mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe na majeruhi ambao ni dereva na wasaidizi wa makamu rais, wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Ligula.
Kabla ya ajali hiyo, gari jingine lililokuwa limebeba baadhi ya waandishi wa habari, Channel ten, Clouds tv na Star TV iliacha njia na kugonga kwenye kingo za barabara lakini hakuna aliyepata madhara.