Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano wafariki dunia mapigano ya wakulima, wafugaji Tanga

Baadhi ya miili ya wananchi wa kijiji cha Elerai na Kibirashi  Wilayani ikiwa tayari kusafirishwa kwenda kuhifadhiwa baada ya kuuwawa  katika mapigano ya wakulima na wafugaji yaliotokea leo Januari 30 wilayani Kilindi mkoani Tanga. Picha na Rajabu Athumani.

Muktasari:

  • Mgogoro huo kati ya wakulima na wafugaji wa eneo la Elerai na Kibirashi umedumu kwa miaka 20 sasa, ambapo wananchi wameiomba serikali kuutafutia ufumbuzi wa kudumu.

Kilindi. Watu watano wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na kukatwa mapanga huku wengine watatu wakijeruhiwa kufuatia mapigano ya wakulima na wafugaji yaliotokea Wilayani Kilindi mkoani Tanga katika kijiji cha Kibirashi na Elerai.
Wakielezea chanzo cha mapigano hayo mashuhuda wa tukio hilo wamesema ni mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wakulima na wafugaji wa vijiji hivyo ambao vuguvugu zake zilianza muda mrefu bila kupata ufumbuzi wa kudumu, ambapo leo Januari 30 ndio ikatoa tukio la mapigano katiya pande hizo mbili.

Mkulima Richard Masaki amesema waliona vijana jamii ya kimasai wakiingia katika eneo lao na kuanza kuwashambulia, kwa kuwapiga na baadae yakaanza mapigano ya mapanga na risasi hadi kutokea vifo hivyo.

Aidha mfugaji David Kimaki amesema ampoteza mjukuu wake Betina ambae ameuwawa kwa kukatwa na Panga katika shambulio hilo.

"Tulivyopita mbele kidogo tukashambuliwa kwa risasi, nikajua ni wale wale watu  nikachukua hatua nikampigia OCD kumpa taarifa kwamba huku kuna mauaji mengine, tukaongozana na kuona miili mingine zaidi", amesema Kimaki.
Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama akiwa eneo la tukio licha ya kuongoza zoezi la kukusanya miili ya marehemu amesema watu watano wamefariki dunia na watutu kujeruhiwa, kutokana na tukio hilo.
Aidha amezitaka pande zote mbili kusitisha mapigano na kusalimisha silaha zao ili utatuzi wa mgogoro huo ufanyike kwa njia ya amani kwani njia wanayotumiwa hawawezi kupata utatuzi.

"Wito ninaotoa kwa pande zote mbili zinazozingamana hapa ni kuacha mapigano haya haraka, kwani mapigano haya hayawezi kusaidia katika kutafuta ufumbuzi na waweke silaha zao chini", amesema DC Busalama.