Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watahiniwa 566,840 kuanza mtihani kidato cha nne kesho

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi

Muktasari:

Baraza la Mitihani la Tanzania limesema maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne utakaonza kesho katika maeneo mbalimbali yamekamilika huku likiwataka wasimamizi kulinda haki za watahiniwa.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limesema jumla ya watahiniwa 566, 840 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne, utakaoanza kesho Jumatatu katika shule za Tanzania Bara na Zanzibar.

  

Limesema kati yao watahiniwa  533,001  ni shule na 31, 839 wa kujitegemea .Kati ya hao watahiniwa wavulana ni  247,131 sawa na asilimia 46.19 na wasichana 287,870 sawa na asilimia 53.81.


Kaimu Katibu Mtendaji  wa Necta, Athuman Amasi, ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 12, 2022 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mtihani huo, akisema kila kitu kinakwenda vizuri ikiwemo mitihani kufika kwenye mikoa na vituo husika.


Amasi amesema katika idadi hiyo wapo watahiniwa wenye mahitaji maalumu 852 kati ya 480 wana uhoni hafifu, 62 wasioona, 19 wenye ulemavu wa kusikia, 152 wenye mtindio wa akili na 139 wana ulemavu wa viungo.


"Mwaka 2021 idadi ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 538,024 hivyo kuja ongezeko la jumla ya watahiniwa 28,816 sawa na asilimia 5.36 kwa mwaka 2022 ukilinganisha na mwaka 2021.


"Maandalizi ya mtihani huu wa kesho yamekamilika ikiwa ni pamoja kusambazwa kwa mtihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani katika mikoa ya Tanzania na Zanzibar," amesema Amasi.


Amasi amesema mtihani wa kidato cha nne ni muhimu kwa wanafunzi na jamii  kwa sababu ina pima umahiri wa wanafunzi katika masomo yote aliyojifunza kwa muda wa miaka minne.Pia amesema matokeo ya mtihani huo yanatumika katika chaguzi za wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu ya sekondari na fani mbalimbali