Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasafiri sasa kukata tiketi ya ndege kwa njia ya WhatsApp

Mkurugenzi wa Precision Air akiongea katika hafla ya uzinduzi wa ukataji tiketi za ndege kwa njia ya WhatsApp jijini hapa

Muktasari:

  • Tofauti na matumizi ya tovuti kwa ajili ya kukata tiketi za ndege kwa wateja saliohitsji kujihudumia kwa njia ya mtandao, sasa wataweza kutumia mitandao ya kijamii ya Whatsapp kukata tiketi hizo.

Dar es Salaam.  Wakati ukuaji wa sayansi na teknolojia ukizidi kushika kasi duniani, ndivyo kampuni zinavyozidi kuja na ubunifu wa namna ya kuwafikia wateja wake, kampuni ya Precision Air imefuata mkondo huo kwa kuja na mfumo wa ukataji tiketi kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Mfumo huo uliopewa jina la Swala umezinduliwa leo Julai 26, 2023 na Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi anayeshughulikia Ujenzi, Godfrey Kasekenya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mkurugenzi wa kampuni ya Precision Air, Patrick Mwanri amesema mtu atakayekata tiketi kupitia Swala hatokutana na ugumu wowote kwani njia inayotumika ni kama kuwasiliana na ndugu yake mwingine.

“Unafanya mwenyewe na unapata tiketi yako ndani ya muda mfupi na hiyo ndiyo utakayoonyesha siku yako ya safari ikiwa katika simu, hii ni huduma ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki,” amesema Mwanri.

Amesema mchakato wa kutengeneza mfumo huo ulianza mwaka 2019, lakini uwepo wa ugonjwa wa Uviko-19 ulichelewesha utekelezaji wake, hawakuweza kuuzuia.

“Pia, ukiwa unakata tiketi huku hauna haja ya kutoka kwenda katika huduma za malipo, badala yake mfumo utakueleza moja kwa moja kuweka neno lako la siri na utakapothibitisha muamala wako utapewa tiketi papo hapo.

“Kama huna hela kwenye simu, unapewa namba ya booking ili uweze kujihudumia,” amesema Mwanri.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Uchukuzi, Kasekenya amesema katika dunia ya sasa ya ukuaji wa sanyansi na teknolojia yenye ushindani wa bishara, mtoa huduma ambaye ataweka urahisi katika kumfikia ndiye atakayepata wateja wengi.

“Mtoa huduma atakayepatikana kwa urahisi ndiyo atakayepata wa kuwahudumia kwa urahisi. Katika utoaji huduma suala la muda, gharama na ubora wa huduma ni muhimu na vigezo vya msingi katika uchaguzi wa huduma,” amesema Kasekenya.

Amesema pia uwepo wa huduma hiyo utasaidia kufumbua watu macho juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii yenye tija kwa ajili ya kuongeza kipato chao na kurahisisha utoaji wa huduma zao.