Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapangaji waibua mpya kortini ghorofa lililoporomoka Kariakoo

Muktasari:

  • Novemba 16, 2024 jengo la ghorofa lilianguka katika Mtaa wa Mchikichi na Kongo, eneo la Kariakoo, na kusababisha Vigo vya watu 31. Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara ndani ya jengo hilo wamefungua kesi wakidai fidia ya jumla ya Sh40 bilioni.

Dar es Salaam. Ni kumbukumbuku ambayo bado haijafutika kichwani mwa Watanzania hasa kwa wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo baada ya jengo la ghorofa kuporomoka. Sasa wapangaji wake wamekuja na mpya mahakamani.

Wafanyabiashara hao waliokuwa wamepanga vyumba vya biashara katika jingo hilo lililoanguka katika Mtaa wa Mchikichini na Kongo, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam mwaka 2024, wamefungua kesi ya madai dhidi ya wamiliki wa jengo hilo wakidai fidia ya jumla ya Sh40 bilioni.

Wafanyabiashara waliokuwa wamepanga vyumba vya biashara katika jengo lililoanguka katika Mtaa wa Mchikichini na Kongo, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam mwaka 2024, wamefungua kesi ya madai dhidi ya wamiliki wa jengo hilo wakidai fidia ya jumla ya Sh40 bilioni.

Jengo hilo lililojengwa katika Kiwanja Na. 12, Block 7, eneo la Kariakoo, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, lilianguka Novemba 16, 2024.

Novemba 29, 2024, wamiliki wake walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, inayoketi Kisutu, kwa kesi ya jinai.

Katika kesi hiyo uchunguzi wa awali namba 33633/2024, wanakabiliwa na mashtaka 31 ya kuua bila kukusudia kinyume cha vifungu vya 195 na 198 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu (PC). Kutokana na vifo vya watu hao wakidaiwa kutenda makosa hayo.

Wanadaiwa Novemba 16, 2024 katika mtaa wa Mchikichi na Kongo, eneo la Kariakoo, washtakiwa hao isivyo halali walishindwa kutimiza majukumu yao na kusababisha vifo vya Said Juma na wenzake 30.

Washtakiwa hao katika kesi hiyo ni Leondela Mdete (49) mkazi wa Mbezi Beach, Zenabu Islam (61) mkazi wa Kariakoo na Ashour Awadh Ashour (38) mkazi wa Ilala.

Wakati kesi hiyo ya jinai ikiwa bado inaendelea mahakamani hapo kwa hatua za uchunguzi wa awali kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu ambako ndiko itakasikilizwa na kuamuriwa, wafanyabiashara hao nao wamewafungulia kesi hiyo Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.

Kesi hiyo imefunguliwa na Kanali Naftal Swai, Sultan Dibwe, Dicko Marcus Msigwa, Aurelian Aloyce Msigwa na Christina Elias Snga pamoja na wenzao wengine 45.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Zenabu Abdallah Ismail (mwakilishi wa marehemu Ismail Abdallah Salim), Asour Awadh Ashu¬r (mwakilishi wa marehemu Awadh Ashour Abeid), na Leondela Augustino Mdete.


Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Mohamed Gwae imetajwa leo Jumanne, Aprili 29, 2025 mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na imeahirishwa na Naibu Msajili Rose Kangwa kwa niaba ya Jaji Gwae ambaye alikuwa na dharura, mpaka Mei 29 kwa ajili ya maelekezo maalumu.

Katika kesi hiyo, wadai hao wanaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wawalipe jumla ya Sh40 bilioni kama fidia ya hasara ya uwekezaji na biashara.

Wanadai hasara hiyo ilisababishwa na uzembe wa wadaiwa kwa ujenzi wa sakafu ya chini ya ardhi usioruhusiwa uliofanywa na wadaiwa, kinyume na makubaliano ya upangaji kati yao na wadaiwa uliosababisha jengo hilo kuporomoka.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, kwa nyakati tofauti kuanzia Januari 2023 hadi Desemba 31, 2024, wadai na wadaiwa waliingia katika mikataba (kwa mdomo na kwa maandishi) ya kupanga katika jengo hilo.

Walalamikaji, wakiwa wapangaji wa wadaiwa, waliwekeza na kuendesha biashara mbalimbali yakiwemo maduka ya rejareja na ya jumla katika jengo hilo.

Jumla ya thamani ya uwekezaji na biashara za wadai zilizokuwa zinaendeshwa katika jengo hilo ni Sh40 bilioni.

Wanadai kwa kuvunja masharti na vigezo vya mikataba wa upangaji kati yao wadai na wadaiwa, wadaiwa walifanya kwa uzembe ujenzi wa chini ya ardhi bila idhini ya mamlaka husika.

Hali hiyo wanadai kuwa ilisababisha kuporomoka kwa jengo hilo Novemba 16, 2024, na kuwasababishia hasara ya uwekezaji na biashara zao wadai ndani ya jengo hilo.

Wanadai kuwa wamekuwa wakidai mara kwa mara wadaiwa wawalipe Sh40 bilioni kama fidia kwa hasara hiyo ya uwekezaji na biashara yao, iliyosababishwa na uzembe wa wadaiwa katika ujenzi huo, uliosababisha kuporomoka kwa jengo hilo.

Hata hivyo wanadai kuwa wadaiwa wamekataa kwa ukaidi kujibu madai yao bila sababu za msingi kisheria au za a haki.

Hivyo wanaiomba mahakama itamke kuwa wadaiwa, kwa kuvunja mikataba ya upangaji kati yao na wadai, walifanya kwa uzembe na bila idhini ujenzi huo wa jengo hilo na kusababisha hasara kwa uwekezaji na biashara zao wadai zilizokuwa zinaendeshwa ndani ya jengo hilo.

Pia wanaomba malipo ya fidia maalum kiasi cha jumla ya Sh40 bilioni, malipo ya fidia ya hasara ya jumla kwa kadri mahakama itakavyotathmini, gaHrama za kesi na nafuu nyinginezo ambazo mahakama itaona zinafaa.