Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapangaji sasa kumiliki nyumba za NHC

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu

Muktasari:

Akizungumzia sera hiyo inayofahamika kama ‘Mpangaji Mnunuzi’, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu amesema sera ya Mnunuzi Mpangaji (Tenant Purchase Scheme),  itamsaidia mnunuzi kumiliki makazi baada ya muda wa malipo kukamilika.

Dar es Salaam.  Utaratibu mpya wa mpangaji kuweza kununua nyumba ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), umeanzishwa utakaomwezesha kulipia kidogo kidogo kila mwezi.

Akizungumzia sera hiyo inayofahamika kama ‘Mpangaji Mnunuzi’, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu amesema sera ya Mnunuzi Mpangaji (Tenant Purchase Scheme),  itamsaidia mnunuzi kumiliki makazi baada ya muda wa malipo kukamilika.

Nyumba hizo amesema zimejengwa kwenye mikoa zaidi ya 15 nchini ikiwamo Geita, Katavi, Dodoma, Kagera na Njombe.

Amesema utaratibu huo umeanza kutumika mwezi huu na muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi mkoa ilipo nyumba anayoihitaji.

Mchechu amesema sifa kuu ya mnunuzi mpangaji ni awe na mshahara au kipato kinachozidi Sh500,000 kwa mwezi na atahitajika kulipa malipo ya awali ya asilimia 25 pamoja na kodi.

“Kiwango cha riba ni asilimia 15 ya kiwango kilichosalia kuwekwa. Mnunuzi atahitajika kulipa malipo kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja kulingana na thamani ya nyumba,” amesema na kuongeza kuwa, kiwango cha malipo cha juu ni miaka 10 au miezi 120 na bei za nyumba ni kati ya Sh29 milioni na Sh49 milioni bila kodi