Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne kizimbani kwa kumwibia mwajiri lita 7, 000 za dizeli

Muktasari:

Wafanyakazi wanne wa Kampuni ya JV Spek LTD inayojenga mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Igunga wakikabiliwa na shtaka la wizi wa lita 7, 441 za mafuta ya dizeli yenye thamani ya Sh20 milioni.

Tabora. Wafanyakazi wanne wa Kampuni ya JV Spek LTD inayojenga mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Igunga wakikabiliwa na shtaka la wizi wa lita 7, 441 za mafuta ya dizeli yenye thamani ya Sh20 milioni.

Mbele ya Hakimu mfawidhi wa Wilaya Igunga, Ludia Ilunda, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo katika siku tofauti kati ya Mei 01, 2023 na Juni 18, 2023 wakiwa maeneo ya Kata ya Nanga Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Akisoma hati ya mashtaka leo Julai 3, 2023, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Ellymajid Kweyamba amewataja washtakiwa kuwa ni waongoza mitambo Ally Said (36), Samwel Mtenga (35), Awadh Mrango (36) na Zuberi Pastory Ally ( 41) ambaye ni dereva.

‘’Wakiwa waajiriwa wa Kampuni ya JV Spek LTD ambayo ni mkandarasi wa ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanzania, washtakiwa waliiba lita 7, 441.94 za mafuta ya dizeli yenye thamani ya Sh20.093 milioni na kuisabababishia hasara kampuni hiyo,’’ amesema Kweyamba

Amesema washtakiwa wote wanne walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 258 (1) 271 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 mapitio ya mwaka 2022.

Washtakiwa wamekana mashtaka dhidi yao na shauri hilo kuahirishwa hadi Julai 31, 2023 itakapotajwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali baada ya upande wa mashataka kuieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo tayari umekamilika. Washtakiwa wapo nje kwa dhamana ya Sh5 milioni kwa kila mmoja.