Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake wachuuzi wa dagaa wabuni mbinu kujiongezea kipato

Wachuuzi wa dagaa, wake kwa waume wakiendelea na shuguli zao za kila siku katika mwalo wa Mswahili jijini Mwanza kabla haujafungwa kwa muda kuruhusu samaki kuzaliana. Picha ya chini ni muonekano wa mwalo huo ukiwa tupu baada ya shughuli za uvuvi kusitishwa kuanzia Machi Mosi, 2023 hadi Machi 14, 2023. Picha na Saada Amir

Muktasari:

Wanawake wachuuzi wa dagaa katika Mwalo la Mswahili jijini Mwanza wamelazimika kubuni mbinu mbadala wa kujiingizia kipato pindi shughuli za uvuvi zinapositishwa kuruhusu samaki kuzaliana wakati wa mbalamwezi.

Mwanza. Wanawake wachuuzi wa dagaa katika Mwalo la Mswahili jijini Mwanza wamelazimika kubuni mbinu mbadala wa kujiingizia kipato pindi shughuli za uvuvi zinapositishwa kuruhusu samaki kuzaliana wakati wa mbalamwezi.

Kwa mujibu wa sheria na kanuni za uvuvi namba 66 kifungu cha (mm) na marekebisho yake ya 2020, shughuli za uvuvi wa dagaa hairuhusiwi wakati wa mbalamwezi.

Katika utekelezaji wa sheria na kanuni hiyo, shughuli za uvuvi wa dagaa katika mwalo maarufu wa Mswahili jijini Mwanza zimesitishwa kwa siku 14 kuanzia juzi Machi Mosi, 2023 hadi Machi 14, zitakaporuhusiwa tena.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Usimamizi wa Maeneo ya Fukwe (BMU), Mwalo wa Mswahili, Lukas Kisibo, mwalo huo una wachuuzi wa dagaa zaidi ya 100, wengi wao wakiwa wanawake. Mwalo huo hutembelea na zaidi ya watu 250 kila siku kwa shughuli mbalimbali ikiwemo biashara na uchuuzi wa bidhaa za samaki.

Sehemu kubwa ya wachuuzi wa mazao ya samaki katika mwalo huo na mialo mengine kadhaa za Ziwa Victoria ni wanawake ambao awali walijikuta njia panda kwa kukosa kipato shughuli za uvuvi zinapositishwa.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Machi 3, 2023, Kagori Swed, mmoja wa akina mama wachuuzi wa dagaa mwalo wa Mswahili amesema amelazimika kuanzisha biashara ya kuuza mihogo mibichi kama njia mbadala wa kujiingizia kipato mwalo unapofungwa.

“Mwalo ulipofungwa mwezi Februari sikuwa nimejiandaa kwa njia nyingine ya kipato, hali iliyosababisha nitumie fedha zangu zote za akiba hadi mtaji kwa mahitaji ya kila siku ya familia. Mwezi huu wa tatu nimejifunza ndio maana unaona ninatembeza miogo mibichi kama njia mbadala wa kipato,” amesema Kagori

Mchuuzi mwingine wa dagaa mwalo wa Mswahili, Monica Marco naye ameitumia ujanja huo wa kuanzisha biashara mbadala kujiingizia kipato wakati shughuli za uvuvi wa dagaa zinapositishwa wakati wa mbalawezi kwa kujiingiza kwenye shughuli ya kuponda na kuuza kokoto.

“Japo wateja wa kokoto siyo wengi kila siku kulinganisha na wale wa dagaa, lakini angalau naweza kuingiza kipato cha kujikimu mimi na familia yangu ya watoto watano,” amesema Monica.

Akizungumzia shughuli za uvuvi kusitishwa kwa muda nyakati za mbalamwezi, Msemaji wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu), Sijaona Kaloli amesema kusitisha shughuli za uvuvi kwa siku 14 nyakati za mbalamwezi ni muhimu kulinda mazao ya samaki.

“Nyakati za mbalamwezi, samaki wanapanda juu kutafuta chakula; hivyo, kuruhusu uvuvi nyakati hizo ni kuruhusu samaki wanaokuja juu juu kutafuta chakula wavuliwe,” amesema Kaloli

Mkoa wa Mwanza, kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Tafu, Jephta Machandalo, unakadiriwa kuwa na zaidi ya wavuvi 30,000.