Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake kujengewa uwezo wa kibiashara

Muktasari:

  • Kuwepo kwa mitaji kwa wafanyabiashara wanawake ni suala moja lakini kuweza kuisimamia imetajwa kuwa ni changamoto kubwa kwa kundi hilo kutokana na kukosa elimu na ujuzi katika usimamizi wa fedha.

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha kundi kubwa la wanawake lililopo kwenye sekta ya biashara linafanya shughuli zao kwa tija, Benki ya Equity Tanzania imesaini mkataba na Taasisi ya ADC Tanzania kwa lengo kuwajengea uwezo katika biashara zao.

Mkataba huo umesainiwa jana Novemba 5, 20204 ambapo utawasaidia wanawake kupata ushauri wa kibiashara ili kuwawezesha kiuchumi. Mradi huu unafanyika kwa ushirikiano na Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa ya African Guarantee Fund/AFAWA.

Lengo kuu la mradi huu ni kuwajengea wanawake uwezo katika biashara zao ili waweze kufikia vigezo vya kupata huduma mbalimbali za kifedha, ikiwemo mikopo inayotolewa na Benki ya Equity, ili kuboresha maisha yao kijamii na kiuchumi.

Aidha, mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Benki ya Equity wa kuongeza wigo wa huduma kwa wateja wadogo na wa kati (MSMEs), kwa lengo la kufikia 65% ya mikopo yote ifikapo mwaka 2030.

"Tukiwa na dhamira ya kuwawezesha wanawake katika biashara, ushirikiano huu ni hatua muhimu ya kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wanawake wajasiriamali na kuwawezesha kufikia ukuaji wa kiuchumi endelevu," amesema Leah Ayoub, Meneja Mkuu wa Biashara wa Benki ya Equity Tanzania.

Mradi huu unalenga kuwawezesha zaidi wanawake nchini Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya elimu ya fedha, mikopo nafuu, na ushauri maalum wa biashara.