Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi wamsubiri Rais Samia Chato

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Chato wakiwa kwenye viwanja vya hospital ya Kanda ya Chato wakimsubiri Rais Samia Suluhu Hassan.

Muktasari:

Tayari viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na mamia ya wananchi wamekusanyika katika viwanja vya hospitali ya Kanda Chato wakimsubiri Rais Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kutembelea hospitali hiyo na kuzungumza na wananchi.

Chato. Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na mamia ya wananchi wamekusanyika katika viwanja vya hospitali ya Kanda Chato wakimsubiri Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anaYetarajiwa kutembelea hospitali hiyo na kuzungumza nao.

 Rais Samia anatokea mkoani Kagera alikokuwa na ziara ya siku mbili ambapo jana Oktoba 14 alihitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kuzungumza na wananchi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (wa pili kushoto), Waziri wa Madini Doto Biteko "(wa pili kulia), Mbunge wa Chato Merdad Kalemani (wa kwanza kulia) na Mbunge wa Geita mjini Constantine Kanyasu (wa kwanza kushoto) wakibadilishana mawazo katika viwanja vya hospital ya Kanda Chato wakati wakimsubiri Rais Samia Suluhu Hassan. Picha na Rehema Matowo

Akiwa wilayani Chato Rais Samia anatarajiwa kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kanda ya Chato pamoja na taarifa ya huduma za kibingwa za matibabu zinazotolewa hospitani hapo na baada ya hapo atatembelea kuona hatua zilizofikiwa.

Hospitali hiyo iliyoanza kujengwa mwaka 2017 awamu ya kwanza ya ujenzi iliyohusisha majengo manne imekamilika na kugharimu Sh16.72 bilioni na awamu ya pili inatarajiwa kugharimu Sh18.5 bilioni ikihusisha jengo la mionzi, wodi ya vitanda 201, hewa tiba pamoja na kazi za nje ikiwamo maegesho ya magari ambapo tayari Serikali imetoa Sh9 bilion.

Hospitali hiyo ina eneo lenye ukubwa wa ekari 248 na hadi sasa zimetumika 18 na itakuwa na vitanda 800 na kuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 700-1000 kwa siku.

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Chato wakiwa kwenye viwanja vya hospital ya Kanda ya Chato wakimsubiri Rais Samia Suluhu Hassan.

Akiwa njiani kwenda wilaya ya Geita Rais atazungumza na wananchi katika eneo la mji mdogo wa Katoro na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo ya wilaya nzima yenye halmashauri mbili za Geita mji na Geita vijijini kisha kusalimia wananchi wa mji mdogo wa Katoro na Buseresere.