Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi wakaribishwa kufungua kesi kwa njia ya mtandao

Dar es Salaam. Mahakama ya Tanzania inatarajia kuanza rasmi kurekodi mwenendo wa kesi kwa njia ya kielektroniki, baada ya kumalisha maandalizi ya matumizi ya mfumo mpya wa Usimamizi wa Mashauri kwa Njia ya Kielekitroniki unaojulikana kwa lugha ya kitaalamu kama e-Case Management System (e-CMS), huku wananchi wakikaribishwa kufungua mashauri ya majaribio kwa njia ya mtandao.

Taaarifa ya Mahakama iliyotolewa na kusainiwa na Kamimu Msajili Mkuu, Sylvester Kainda kwa niaba ya niaba ya Msajili Mkuu wa Mahakama, mfumo huo mpya unatarajiwa kuanza kutumika rasmi kuanzia Novemba Mosi 2023 baada ya kukamilika kwa majaribio mwishoni mwa mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa leo, Jumatatu, Oktoba 16, 2023, mfumo huo ni sehemu ya maboresho yanayofanywa na Mahakama ya Tanzania katika maeneo mbalimbali lengo kwa lengo la kuboresha huduma za upatikanaji wa haki kwa wakati na kwa gharama nafuu kwa wananchi.

Kainda amesema katika taarifa hiyo kuwa mfumo huo mpya unachukua nafasi ya mfumo wa awali wa Menejimenti ya Mashauri yaani JSDS2, ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 2018.

“Ujenzi wa mfumo huu unalenga kuongeza tija katika shughuli za kimahakama, kupunguza gharama za usikilizaji wa mashauri kwa upande wa mahakama na wananchi, kupunguza muda wa kusikiliza mashauri na kusogeza zaidi huduma za kimahakama karibu na wananchi,” amesema Kainda.

Pia amesema kuwa matumizi ya mfumo wa e-CMS unalenga pia kutatua changamoto mbalimbali za mfumo wa JSDS2 zikiwemo kuongezeka kwa watumiaji na matumizi ya mfumo yasioendana na muundo wa awali wa mfumo na tekinolojia iliyotumika kuujenga, kutoruhusu mienendo ya mashauri kuandikwa moja kwa moja kwenye mfumo.

“Mfumo mpya wa usimamizi wa mashauri kwa jjia ya kielekitroniki" e-Case Management System" pia utarahisisha usajili wa mashauri kwa njia ya mtandao, upangaji wa mashauri kwa Majaji na Mahakimu, utaruhusu mienendo ya mashauri kuandikwa moja kwa moja kwenye mfumo na kuihifadhi kielektroniki,” amesema.

Baadhi ya mawakili ambao ni miongoni mwa wadau wa mahakama waliozungumza na Mwananchi wameunga mkono matumizi ya mfumo huo huku wakitoa changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi au kutatuliwa na mfumo huo mpya, zinazojitokeza katika mfumo unaotumika sasa wa JSDS2.

Wakili Edson Kilatu amesema kuwa kuletwa kwa mifuno kama hiyo kunaongeza uwazi ambao pia unaongeza uwajibikaji.

“Kwa sababu kama mwenendo uko kwenye mfumo, mtu anaweza aka-access (apata fursa ya kuurejea). Kwa hiyo hata uwezekano wa mashaka kwamba wakati mwingine mtu anaweza akachezea mwenendo yanakuwa hayapo.

Hata hivyo amesema kuwa wasiwasi wake ni kwamba hata huu mfumo wa sasa bao una changamoto nyingi ambazo hazijapatiwa majibu, huku akizitaja kuwa ni pamoja na tatizo la mtandao akifafanua kuwa kuna wakati wanaweza kuingia kwenye mfumo lakini wakakuta kuna tatizo la mtandao.

“Je internet (mtandao) ni tatizo la mfumo wenyewe au ni kwamba mfumo wetu wa internet una matatizo. Sasa sijui kama mfumo mpya utakwenda kutatua changamoto ya internet pia, ambayo ni iko nje ya taasisi (mahakama) kwa kuwa ni tatizo la kitaifa”, amesema Kilatu na kuongeza:

“Kingine bado unafungua kesi online (mtandaoni) na unalazimika kupeleka hardcopy (nyaraka ngumu- makaratasi) tena. Kwa hiyo unafanya mchakato mara mbili ambao unakuwa ni mzigo. Tulitarajia ukishafungua mtandaoni inakuwa imekamilika labda unawapelekea upande wa pili tu nyaraka.”

Wakili Kilatu amebainisha changamoto nyingine kuwa bado mfumo huo unategemea ushiriki wa mtu (msajili), ambapo inachukua muda kusajiliwa na kwamba wakati mwingine mpaka wanapiga simu ndipo wanaifanyia usajili.

Hivyo amesema kuwa wanatarajia mfumo uwe na uwezo wa kuisajili kesi wenyewe moja kwa moja mara tu inapokuwa imefunguliwa mtandaoni bila kutegemea tena mtu na kwamba kesi ikishalipiwa tu moja kwa moja na kwenye mfumo unaonesha.

Kwa upande wake ofisa sheria kutoka kampuni ya Bemora Attorneys, David Kahabi amesema kuwa mfumo huo utaweza kuwa na tija iwapo tu umeandaliwa vyema na wadau na watendaji wamejiandaa kuutumia kwa tija na kuwa na ulinzi wa kumbukumbu zisiweze kushambuliwa na virusi.

Kahabi amesema kuwa hata katika mfuno wa sasa kuna usumbufu mkubwa kutokana na tatizo la mtandao kuwa chini jambo ambalo linasababisha kutumia muda wa siku mbili mpaka tatu kwa kesi kusajili tangu inapofunguliwa kielektroniki hivyo kusababisha msongamo wa mashauri yanayosubiri kusajiliwa.

Kuhusu mwenendo wa kesi kurekodiwa kielektroniki, Kahabi amesema hilo ni jambo zuri kwa kuwa litamsaidia hakimu au jaji wakati anapoandika hukumu kujikumbusha kile kilichosemwa na pande zote kwa usahihi na hivyo kutenda haki.

“Lakini hilo linaweza kuwa na tija kama tu kumbukumbu hizo hazitaharibiwa na virusi na kusababisha kumbukumbu hizo kuharibika,” amesisitiza Kahabi.

Hata hivyo, Kainda katika taarifa hiyo amefafanua zaidi kuwa mfumo huo umekuja na muundo na tekinolojia ya kisasa inayoendana na mahitaji ya sasa ya Mahakama na wadau wake.

Amebainisha kuwa mfumo huo unaweza kusomana na mifumo mingine ya ndani ya Mahakama na ile ya wadau wake muhimu kama Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), na taasisi nyinginezo.

“Hatua hii itarahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kutoka taasisi hizo na kuwezesha wadau hao kupata taarifa mbalimbali za mashauri kwa urahisi,” amesema Kainda.

Kutokana na matumizi ya mfumo huo Kainda amesema kuna fomu maalumu (template) za nyaraka mbalimbali zinazotumika mahakamani zikiwemo hati za shauri, hati za mashtaka, hukumu zitakazojazwa na watumiaji ndani ya mfumo.

Amesema kuwa majaribio ya mfumo huo mpya wa e-CMS yalianza Oktoba 2, 2023 katika mahakama zote nchini na yanaendelea mpaka Oktoba 31, kabla ya kuanza matumizi rasmi Novemba Mosi.

Hivyo amewaalika wananchi na wadau wa mahakama kufungua mashauri ya majaribio kwa wingi kwenye mfumo huo maalumu wa majaribio unaopatikana kupitia anwani https://cmstrainingjudiciary.go.tzl.

Hata hivyo, Kainda amesema kwamba kwa wale wenye akaunti katika mfumo wa JSDS2, wanaweza kuingia katika mfumo huo mpya kwa kutumia taarifa za akaunti zao za JSDS2.

Amesema kuwa wale watakaotaka msaada zaidi juu ya namna ya kuufikia au kutumia mfumo huu, wanaweza kuwasiliana au kufika katika madawati maalumu ya kuwasaidia wateja yaliyopo katika mahakama zote nchi nzima.

“Kipindi cha majaribio kitaendelea hadi 31 Octoba 2023 kwa lengo la kupata changamoto zitakazojitokeza katika matumizi ya mfumo huo ili ziweze kufanyiwa kazi kabla ya kuanza kutumika rasmi kwa mfumo huu hapo tarehe 1 Novemba, 2023,” amesema Kainda na kuongeza:

“Hivyo, kwa mtumiaji yeyote atakayepata changamoto yoyote au mwenye maoni kuhusu matumizi ya mfumo huu basi aitume changamoto hiyo au maoni hayo kwenye barua pepe [email protected]. Shughuli za majaribio ya e-CMS hazitaathiri huduma za Mahakama kupitia JSDS2.”


Hata hivyo Kainda amesema kuwa katika kipindi hicho cha majaribio, ufunguaji wa mashauri kwa njia ya JSDS2 utaendelea na Mahakama itashughulikia changamoto zote zitakazo jitokeza kwenye mfumo huo hadi pale mfumo huo utakapokoma rasmi kutumika tarehe 1 Novemba 2023 triakapoanzakutumia e-CMS.

Pia amebainisha kuwa matumizi ya e-CMS yatakapoanza rasmi madirisha yake ya msaada kwa wananchi (viosk) wasioweza kutumia wenyewe JSDS2 yataendelea kutumika pia kutumika katika mfumo huo wa e-CMS.