Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanakijiji wahamasika matumizi ya vyoo bora

Moja kati ya choo walivyojenga wananchi wa kitongoji cha Namangale baada ya kuhamasishwa kujenga vyoo bora na kuacha tabia ya kujisaidia vichakani. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Mradi wa kuimarisha hali ya usafi wa mazingira ngazi ya jamii unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la nchi ya Korea-CCK na kutekelezwa Heart to Heart umewezesha wanavijiji kujenga vyoo bora na kuwaepusha na magonjwa.

Lindi. Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Namangale mkoani hapo wamesimulia namna walivyoachana na utamaduni wa kutotumia vyoo.

Wanakijiji hao walizungumza hayo leo Desemba 2, 2023 walipotembelewa na Ofisa mradi wa kuimarisha hali ya usafi wa mazingira ngazi ya jamii unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la nchi ya Korea-CCK na kutekelezwa Heart to Heart kijiji hapo.

Ashura Ally Hassan mkazi wa kijiji cha Namangele ambaye ni mjumbe wa kamati ya uhamasishaji wa wananchi kujenga vyoo alisema kuwa awali hali ilikuwa mbaya.
Amesema kuwa wapo wananchi ambao walikuwa na hawana vyoo majumbani mwao na walikuwa wakijisaidia popote bila kujali usalama wao.

“Elimu  kuhusu usalama wa afya zao ilikuwa ndogo, waliathiri kiafya  na kisaikolojia.
“Ujue hawa watu walikuwa wakijisaidia popote nikisema popote namaanisha kwa kweli hali ilikuwa mbaya, ila kwa sasa kadri tunavyotoa elimu tunaona mabadiliko kwakuwa tunawajenga kisaikolojia na wengi wamehamasika kujenga vyoo bora,” amesema Hassan.

Naye Ally Dunia mkazi wa kijiji cha Namangale amesema kuwa ilibidi kuhamasisha na kutembelea kila nyumba ili kuhakikisha kuwa kila kaya inakuwa na choo bora chenye kibuyu chilizi, ambacho kitasaidia kunawa anapotoka kujisaidia.

Mfano kipindi hiki cha masika unaweza kuingia bafuni na ukaoga na unakuwa na amani, lakini ukiingia kwenye choo kisichoezekwa ni changamoto kubwa huwezi kukitumia wakati wa masika,” amesema Dunia.

Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Namangele, Wakati Kambanga amesema kuwa wengi walijua choo ni shimo tu. Ila choo bora kinatakiwa kuwa na sifa tano ambazo ni shimo, ukuta, paa, mlango na mfuniko.

“Magonjwa yalikuwepo ila hatukujua kama kutotumia vyoo bora ndiyo sababu.

“Watu waliharisha damu na wengine kawaida lakini hatukujua yanatokana na nini sasa hivi kulingana na elimu tuliyopata hakuna mwananchi anaweza kwenda porini kujisaidia,” amesema Kambanga.
 

Akizungumzia mradi huo, ofisa mradi wa Shirika la Heart to Heart, Eston Waliha amesema kuwa mradi huo uliibuliwa ili kuchagiza hali ya usafi.

Amesema kuwa kaya nyingi hazina vyoo katika maeneo hayo, lakini pia ilionekana kuwa jamii nyingi ina tamaduni ya kujisadia maeneo ya wazi.

“Kitendo cha kujisaidia hovyo kila mahali bila utaratibu inapotokea mvua inakuwa rahisi kinyesi kuchukuliwa mpaka kwenda kwenye vyanzo vya maji. “Kibaya zaidi jamii nyingi hazina  tamaduni za kuchemsha maji ya kunywa, hivyo kuweka afya zao shakani,” amesema Waliha.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mtama, Dk Dismas Masulubu amesema kuwa zaidi ya asilimia 58 ya kaya zina  vyoo, ambapo kwa sasa mradi upo katika vijiji vya Namangale na Mandiwa ili kuhakikisha kuwa kila kaya inakuwa na choo bora.

“Kwa Halmashauri ya Mtama tumeanza kuhakamsisha wananchi ili kuwa na vyoo bora lengo letu tunataka kila kaya iwe na vyoo bora, ili kuondoka na watu kujisaidia hovyo ili kudhibiti magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira,” amesema Dk Masulubu