Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi 56,132 waanza kunufaika mikopo elimu ya juu

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 20, 2023 jijini Dar es Salaa.

Muktasari:

  • Jumla ya wanafunzi 56,132 wamepangiwa mikopo ya Sh159.7 bilioni katika awamu ya kwanza baada ya Serikali kutenga Sh731 bilioni kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Dar es Salaam. Ni vicheko kwa wanafunzi 56,132 waliopangiwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini baada ya kupangiwa mikopo ya elimu ya juu katika awamu ya kwanza inayoenda sambamba na nyongeza ya fedha za kujikimu kutoka Sh8, 500 hadi Sh10, 000.

 Itakumbukwa kuwa Februari mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alipokutana na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) alipokea ombi la kuongezwa kwa fedha za kujikumu na kuahidi kuwa itaongezwa kufikia Sh10, 000.

Akizungumza leo Oktoba 20, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru amesema kiasi cha Sh159.7 bilioni kimetolewa kwa wanafunzi hao waliopangiwa mikopo katika awamu ya kwanza.

Amesema orodha ya awamu ya pili ya mikopo itatolewa Oktoba 27, lengo likiwa ni kutoka mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 75000 katika mwaka wa masomo 2023/2024.

“Orodha hii ya kwanza inajumuisha wanafunzi wenye sifa zikiwemo kuwa wahitaji, wameomba kwa usahihi na wamekamilisha taratibu za udahili wa chuo kimoja. Tunakamilisha uchambuzi wa maombi menhine na tutaoa orodha ya awamu ya pili,” amesema Badru.

Kuhusu wanafunzi wanaoendelea alisema 145,376 watapata mikopo hiyo na kufanya jumla ya wanufaika kwa mwaka huu kuwa 220,376 ambapo jumla ya Sh731 bilioni zimetengwa kwa ajili hiyo.


Mkurugenzi wa upangaji na utaoji mikopo wa HESLB, Dk Peter Mmari amebainisha kujirudia kwa makosa yanayofanywa na waombaji ikiwemo kutowasilisha nyaraka sahihi na kutofuata maelekezo yaliyotolewa katika mwongozo wa uombaji mikopo.

 “Kuna changamoto tunaziona na tumepanga kutoa taarifa rasmi inayoonesha sababu zilizowafanya wengine wakose mikopo, kwa sasa tunaendelea na uchakati wa maombi yaliyopo ili ifikapo Oktoba 27 awamu ya pili itoke,” amesema Dk Mmari.

Akizungumzia hatua hiyo rais wa Tahliso, Maria John amewataka wanafunzi kutumia vyema fedha wanazopewa kwa kuwa lengo ni kurahisisha maisha yao wanapokuwa vyuoni ili waweze kutimiza kilichowapeleka.

“Tuliomba fedha za kujikimu ziongezwe, Serikali imesikia na imeziongeza sasa zikatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa na zitumike kwa uangalifu mkubwa. Kupata mkopo haina maana ukatumie hovyo kama ambavyo wanafanya wengine tunawaona huko vyuoni,” amesema Maria.