Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi 522 Simanjiro kufanya mtihani wa kidato cha sita kesho

Muktasari:

  • Wanafunzi hao 522 wa kidato cha sita wanatoka kwenye shule nne za sekondari Simanjiro, Naisinyai, Mgutwa na Emboreet wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara


Simanjiro. Wanafunzi 522 wa kidato cha sita wa shule nne za sekondari wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu hiyo inayoanza kesho Mei 5, mwaka 2025 nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Gracian Makota akizungumza na Mwananchi leo Mei 4, 2025 amesema maandalizi yote ya yamekamilika.


Makota amesema wanafunzi hao 522 wanatoka kwenye shule nne, tatu za Serikali na moja ya binafsi.

Amezitaja kuwa, ni Simanjiro iliyopo Kata ya Orkesumet, Naisinyai ya Kata ya Naisinyai na Emboreet ya Kata ya Emboreet na shule binafsi ya Mgutwa iliyopo  Shambarai.

Mkurugenzi huyo amesema kati ya wanafunzi hao 522 wavulana ni 449 na wasichana ni 73.

"Maandalizi yote yamekamilika kwa wanafunzi na kwa shule zao, tunawaombea kwa Mungu wafanye mitihani yao salama," amesema Makota.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Naisinyai, Simon Siria amewatakia kila la heri wanafunzi 290 wa shule hiyo ambao wanaingia kwenye mitihani hiyo.

“Naimani kila mwanafunzi atakayefanya mitihani hii anatambua wajibu wake, hatarajii kusikia mambo mabaya dhidi yao, na imani yangu kwao ni matokeo mazuri,” amesema mwenyekiti huyo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Simanjiro, Thomas Nko amesema wanafunzi 53 wa shule hiyo wanaotarajia kufanya mtihani huo, wameandaliwa vyema na shule kazi imebaki kwao kufanya vizuri.

"Kama ni kusoma wamesoma vya kutosha wanafunzi tumewafundisha vema kinachosubiriwa ni mtihani pekee hivi sasa na nawatakia kila la heri kwao," amesema Nko.

Meneja wa Shule ya Sekondari Mgutwa, Monica Mlemeta amewatakia kila la heri wanafunzi wote watakaofanya mtihani huo kuanzia kesho.

"Shule yetu ya Mgutwa ni miongoni mwa shule nne za sekondari za kidato cha sita katika Wilaya ya Simanjiro, ambazo wanafunzi wake wanafanya mtihani wa kuhitimu," amesema Mlemeta.

Mmoja kati ya wanafunzi wa shule ya sekondari Naisinyai anayeingia kwenye mtihani huo,  Yohana Samson amesema wamejiandaa vyema na wanaushukuru uongozi wa shule kwa walivyowalea.

"Tumesoma kwa bidii kwa muda wote tuliokuwa shuleni hapa na tunatarajia kufanya mtihani wetu vizuri," amesema.