Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliopigana Vita ya Kagera walishalipwa, wakarudishwa makwao

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax akijibu maswali ya wabunge leo Aprili 28, 2025 bungeni jijini Dodoma.

Muktasari:

  • Serikali imesema haina tatizo na wapiganaji wa Vita ya Kagera kwa kuwa, ilishawalipa wote.

Dodoma. Serikali imetangaza kuwa wapiganaji wa Vita ya Kagera na Uganda ambao hawakujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walilipwa kifuta jasho Sh5,000 na kupewa asante na Mwalimu Julius Nyerere (Rais wa Tanzania wa wakati huo) na kurejeshwa makwao.

Kaili hiyo imetolea bungeni leo Jumatatu Aprili 28, 2025 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Rose Busiga.

Mbunge huyo ameuliza ni lini Serikali itawalipa mafao yao mashujaa wa Vita vya Kagera na Uganda. 

Vita ya Kagera ilianza mwaka 1978 hadi 1979 katika Mkoa wa Kagera unaopakana na Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Tanzania.

Majeshi ya Tanzania kwa kushirikiana Majeshi ya waasi Uganda yalimuondoa kiongozi wa kijeshi wa wakati huo nchini Uganda Field Marshal Idd Amin Dada.

Dk Stergomena amesema kundi lililoshiriki vita na halikuwa limeajiriwa na vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya vita lilipewa nafasi ya kujiunga katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kufuata taratibu.

Amesema mashujaa wote waliopigana vita vya Kagera na waliostahili malipo ya viinua mgongo na pensheni walikwishalipwa na wengine wanaendelea kulipwa kwa mujibu wa Sheria ya Pensheni na Viinua Mgongo ya Mwaka 1966, ikiwamo malipo ya ulemavu na kustaafu.

"Kundi ambalo lilishiriki vita na halikuwa limeajiriwa na vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya vita lilipewa nafasi ya kujiunga katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kufuata taratibu,"amesema Dk Stergomena.

Amesema wizara imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali kuhusiana na maveterani wa Vita ya Kagera.

Miongoni mwa changamoto hizo ni madai ya mavetenari wote kuingizwa katika daftari la Pensheni licha ya kuwa, baadhi yao hawakidhi vigezo kwa mujibu wa sheria, madai kuwa pensheni ni ndogo na maombi ya kupewa Bima ya Afya.

Ili kukabiliana na changamoto hizo amesema, wizara imeandaa mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Pensheni na Viinua Mgongo ya mwaka 1966 na kuiwasilisha serikalini, yakijumuisha maveterani waliopigana Vita ya Kagera.

Aidha, Wizara imewasilisha serikalini mapendekezo ya kuona uwezekano wa kuwaingiza Maveterani waliopigana Vita vya Kagera kwenye utaratibu wa Bima ya Afya.