Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliofutiwa matokeo kidato cha nne kurudia mitihani

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda.

Muktasari:

  • Wanafunzi amabo walifutiwa matokeo yao ya kidato cha nne mwaka 2022 wamepewa nafasi ya kurudia mitihani yao ya kumaliza elimu ya sekondari huku shule zilizotajwa kuhusika na udanganyifu zikisalia chini ya uangalizi

Dar es Salaam. Wakati wanafunzi 337 waliofutiwa matokeo yao ya kidato cha nne mwaka 2022 wakipewa nafasi ya kurudia mitihani yao kuanzia Mei 2 mwaka huu, shule zinazodaiwa kufanya udanganyifu kuendelea kusalia chini ya uangalizi.

Wanafunzi hao ambao wanapaswa kuomba kufanya mtihani wa marudio kwa kujisajili kama watahiniwa binafsi (Private Candidate) watafanya mitihani yao sambamba na kidato cha sita watakaokuwa wanamaliza ngazi hiyo ya elimu.

Kati ya watahiniwa waliopewa nafasi hiyo, 333 walifutiwa matokeo kutokana na udanganyifu huku wanafunzi 4 walifutiwa matokeo kutokana na kuandika matusi katika mitihani yao.

Akizungumza jana, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolg Mkenda alisema ikiwa wanafunzi hao wangerudia mitihani na wenzao wa kidato cha nne katika utaratibu wa kawaida kama ilivyozoeleka, Serikali ingepata hasara ya Sh1 bilioni.

“Ila kwa utaratibu huu wa kuomba wenyewe kama Private Candidate na kufanya mtihani huo pamoja na wenzao wanaofanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu kwa utaratibu utakaowekwa na Necta (Baraza la Mitihani la Taifa) basi itasaidia sana kupunguza gharama," alisema Profesa Mkenda.

Amesema kinachofanyoka ni huruma kwani watoto hao wamejikuta wamebananishwa kwenye pembe ya udanganyifu, wamepewa adhabu na kujikuta wanabeba makosa ya taasisi.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka Watanzania kwa ujumla kukemea kwa pamoja matukio ya wizi wa mitihani kwani inafundisha watoto udanganyifu, wizi huku ikiondoa weledi na kuwanyima haki watahiniwa ambao hawajashiriki katika wizi huo ila wamefaulu kwa jitihada zao wenyewe.

"Kufuta matokeo ya mtihani kwa wanafunzi wetu ni uchungu mkubwa kwani kuna baadhi ya wanafunzi watashindwa kurudia mitihani katika duru zinazofuata kutokana na changamoto mbalimbali hasa watoto wetu wa kike na kujikuta wanapoteza ndoto zao,"alisema Profesa Mkenda.

Kuhusu shule zilizohusika katika udanganyifu alisema bado zipo chini ya uangalizi na uchunguzi na utakapokamilika hawatasita kuzifutia usajili kwani Wizara ya Elimu haiwezi kuvumilia shule iliyosajiliwa kugeuka kuwa kiwanda cha udanganyifu.

“Hatutasita wala kuvumilia shule yeyote ambayo imegeuka kiwanda cha wizi na udanganyifu wa mitihani na mbaya zaidi shule hizo zimefanya udanganyifu huo kitaasisi kuonyesha kuwa walijipanga kabisa kwa wizi wa mitihani hivyo baada ya uchunguzi wote kukamilika hatutamfumbia yeyote macho kuanzia shule zenyewe, wasimamizi mpaka Askari waliohusika nao tutawashughulikia kisheria.” Alisema Profesa Mkenda.

Wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne, Athuman Amasi alisema vituo vitatu vimefungiwa kufanya mitihani baada ya kuthibitika kupanga na kufanya udanganyifu.

Alivitaja vituo hivyo ni Andrew Faza Memorial cha Kinondoni Dar es Salaam, Cornelius cha Kinondoni na Mnemonic Academy cha Halmashauri ya Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.