Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakili Mwabukusi, Mdude, waachiwa kwa dhamana

Muktasari:

  • Wawili hao wameachiwa leo jioni kwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Mbeya walipokuwa wameshikiliwa ambapo wametakiwa kuripoti Jumatatu kituoni hapo.

Mbeya. Baada ya kusota rumande kwa takribani siku nane, hatimaye leo Wakili Boniface Mwabukusi na Mwanaharakati Mpaluka Nyangali maarufu Mdude, wameachiwa na Jeshi la Polisi kwa dhamana huku wakitakiwa kuripoti kituoni hapo Jumatatu Agosti 21.

Wawili hao pamoja na kuachiwa kwa dhamana, wamefutiwa kesi iliyokuwa ikiwakabili ya uhaini, badala yake wakishtakiwa na kesi ya uchochezi.

Wakili Philip Mwakilima ambaye anawatetea wawili hao amesema wameachiwa kwa dhamana pamoja na masharti ikiwamo kupata wadhamini wawili kila mmoja, kitambulisho cha Taifa, udhamini wa mali isiyo hamishika yenye thamani ya Sh10 milioni kila mmoja.

"Kesi haijafutwa ndio maana wamedhaminiwa kwa masharti hayo pamoja na kutakiwa kuripoti kituo cha Polisi Jumatatu wakiwa na vitamburisho ambavyo havikuwepo kwa sasa, lakini kesi yao ni uchochezi" amesema Mwakilima.

Wakiongea kwa ufupi, Mwabukusi amesema ndege ikishaanza safari haina ‘reverse’ akimaanisha hairudi nyuma, hivyo hata wao bado mapambano ni yaleyale huku akiahidi kukutana na vyombo vya habari siku watakayoipanga kuweka wazi msimamo wao wa maandamano.

"Kwamba wakituweka Polisi watatukomoa kwa chochote, ndege ikianza safari haina ‘reverse,’ kimsingi tunawashukuru wadau ambao walikuwa sambamba kwa maombi yao juu yetu," amesema Mwabukusi.

Naye Nyagali amesema kwa sasa wanataka kufahamu hatma ya mwenzao Dk Wilbroad Slaa kama naye ameachiwa ili wakutane watatu wapange mwendelezo wao wa kupinga uwekezaji kwenye bandari na maandamano.

"Mimi Polisi ni nyumbani, kunipeleka huko ni sawa na chumbani...tunaenda kukutana na mwenzetu tuwe watatu ili kupanga mwendelezo wetu wa kile tulichokianzisha, hatutishiki," amesema Nyagali.