Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakazi wawili wa Dar wanaswa wakisafirisha mirungi mkoani

Muktasari:

  • Watuhumiwa hao ambao ni Halid Salimu Awadhi (54) dereva mkazi wa Temeke na Yusuph Kondo (46) fundi mkazi wa Bungoni, walikamatwa na mirungi bunda 184 sawa na Kilo 61, ambayo walikuwa wakiisafirisha Toyota X-Trail.

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linawashikilia watu wawili wakazi wa Dar es Salaam, kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni mirungi bunda 184 sawa na kilo 61.

Akizungumza leo Jumatano Aprili 5,2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao Aprili 1, 2023 saa 7:20 mchana katika eneo la Mengwe wilayani Rombo.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Halid Salimu Awadhi (54) dereva mkazi wa Temeke na Yusuph Kondo (46) fundi mkazi wa Bungoni, Dar es Salaam ambapo walikiwa wakisafirisha mirungi hiyo kwenye Gari aina ya Toyota X-Trail.

"Watuhumiwa hao ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam, wakitumia gari aina ya Toyota X Trail, walipofika kizuizi cha Polisi Mengwe, walipekuliwa na kukutwa na mirungi bunda 184 sawa na kilo 6," amesema.

Aidha Kamanda Maigwa amesema, watuhumiwa hao, watafikishwa mahakamani wakati wowote.