Wahoji sababu za mabadiliko Toto Afya Kadi

Muktasari:
- Mabadiliko kwa mfumo wa Toto Afya kadi ya NHIF umeelezwa kufanyika kwa ghafla bila kuwaandaa wazazi na walezi kwa kuwapa elimu ya kutoka na matokeo yake kuzua lawama kwa wananchi.
Dar es Salaam. Mabadiliko kwa mfumo wa Toto Afya kadi ya NHIF umeelezwa kufanyika kwa ghafla bila kuwaandaa wazazi na walezi kwa kuwapa elimu ya kutoka na matokeo yake kuzua lawama kwa wananchi.
Wameyasema hayo leo Septemba 20, 2023 wakati wakichangia mjadala wa Mwananchi X-Space ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd ukiwa na mada ya ‘Mabadiliko ya huduma ya toto afya kadi nini sababu matokeo na suluhsho lake’.
Dickson Ng'hily, Mhariri wa tovuti ya Mwananchi, amesema baada ya kuwa wamesitisha kwanza ilikuwa ghafla kiasi kwamba raia wengi walikuwa hawajui kinachoendelea na hao watoto wanatakiwa kutibiwa mashuleni.
"Sijui kama walifanya mawasiliano ya kutosha na hizi shule, shule anayosoma binti yangu hakukuwa na mpango huo ilinisumbua, kufika hospitali naambiwa hii kadi haitumiki tena na ilikuwa bado haijaexpire hawakututendea haki," amesema Ng'hily.
Amesema ilitakiwa wananchi wawe na taarifa wajue wanapofikia maamuzi wawe wanajua kinachoendelea.
“Watanzania wengi waliwalipia watoto bima lakini wao wahakujilipia, sasa Mtanzania wa kawaida ataipata wapi?” amehoji.
Amesema Waziri wa Afya na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanapaswa kutoa elimu zaidi kwa wananchi juu ya uamuzi wa kuwaondoa watoto kwenye bima ya afya ya toto kadi na kuwaweka kama wategemezi.
Kwa upande wake mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Baraka Loshilaa amesema ili kutimiza masharti ya NHIF, elimu zaidi inatakiwa kutolewa.
“Si watu wote wanajua masuala ya bima wanataiwa kwenda kjijini na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa bima na ukifanikiwa kumsahawishi wanatakiwa kusajiliwa hapo hapo,” amesema.