Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafugaji kuku Songwe walalamikia soko, dawa, chakula

Baadhiya kuku wa kienyeji wakiwa kwenye Banda. Stephano Simbeye

Muktasari:

  • Wamedai kuwa wanafanya hivyo kutokana na kuwa upatikanaji wa chakula kinachozalishwa nchini, ni mgumu na kwamba hata kinapopatikana, huuzwa kwa bei kubwa ikilinganishwa na kile kinachoingizwa toka nchi jirani.

Songwe. Wafugaji wa kuku wilayani Mbozi, mkoani Songwe, wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vifaranga, chakula na dawa za tiba iwapo ukijitokeza ugonjwa.

Hayo yanajiri wakati wafugaji wenzao nchini wamepata hasara baada ya serikali yao kutekeza takriban kuku 45,000 katika harakati za kuzuia kuenea kwa homa ya ndege.

Wakizungumza na Mwananchi Digital kwa nyakati tofauti leo Oktoba 20, 2023; wafugaji hao wamesema kuwa hakuna viwanda vya uzalishaji vifaranga na chakula hali inayowafanya kulazimika kununua chakula toka nchi jirani ya Zambia.

Wamedai kuwa wanafanya hivyo kutokana na kuwa upatikanaji wa chakula kinachozalishwa nchini, ni mgumu na kwamba hata kinapopatikana, huuzwa kwa bei kubwa ikilinganishwa na kile kinachoingizwa toka nchi jirani.

Esnati Nyemba, mkazi wa Ichenjezya amesema kuna uhaba wa chakula kinachozalishwa hapa nchini na hata madukani hakipo, badala yake maduka yote ya vyakula vya mifugo mkoni humo, yanauza chakula kilichoingizwa toka Zambia.

"Mara nyingi tunanunua starter au growers na layers zinazoingizwa toka nchi jirani ya Zambia ambazo pia bei yake ni kati ya Sh65, 000 na Sh75, 000 wakati chakula cha hapa nchini kinauzwa kati ya Sh85, 000 na Sh90, 000,” amesema Nyemba.

Nuru Kayuni ambaye ni mkazi wa Ilolo, yeye amegusia changamoto za ukosefu wa viwanda vya kuzalisha vifaranga, chakula, dawa za tiba na ukosefu wa soko la uhakika la kuku, akisema “vinakwamisha kazi yangu ya ufungaji.”

Amesema kwa sasa ananunua vifaranga toka kimoja kilichopo Iringa ambacho pia hunazalisha chakula, na kwamba kina tawi jijini Mbeya, hata hivyo, amedai upatikanaji wa vifaranga unachukua muda mrefu kwani inabidi usubirie jambo linalokwamisha malengo yake.

"Kuhusu chakula cha vifaranga hao pia kampuni hiyo inazalisha lakini mpaka kifike ukanda wetu huu gharama inakuwa kubwa, ukilinganisha na kinachoingizwa toka nchi ya Zambia, ingawa hiki cha iringa kina ubora mzuri," amesema Kayuni.

Kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa, mfugaji huyo amesema: “Hizi nazo ni changamoto, hazipatikani kwa urahisi, nimekuwa nikipata hasara pale ninapokosa dawa kwani kuku hufa, hata hivyo kwa upande wa chanjo, hizo zipo na zinapatikana kwa urahisi.”

"Kwa Sasa soko tulilonalo ni la ndani, soko hili halitabiriki wakati mwingine kuku wanaadimika sokoni na kutufanya tuuze vizuri lakini wakati mwingine kuku wanakuwa wengi hivyo tunakosa soko zuri" amesema Kayuni.

Kwa upande wake Afisa Mifugo wilayani hapa Aizak Mahai alipotafutwa ili kuzungumzia hali hiyo kwa simu amesema yuko safarini na hivyo kutoa namba ya msaidizi wake ambaye baada ya kupigiwa simu, alimuomba mwandishi wa habari hii kufika ofisini kwake Jumatatu asubuhi ili apatiwe ufafanuzi.