Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara watoa kongole sheria ya uwekezaji

Violet Lusana mfanyabiashara wa mjini Tabora akizungumza katika maonesho ya Nane nane mjini Tabora. Pcha na Robert Kakwesi.

Muktasari:

Sheria mpya ya uwekezaji namba 10 ya mwaka 2022 imewavuta wawekezaji wa ndani wakisema imetoa ahueni kwenye kiwango cha kujiandikisha kwa asilimia 50.

Tabora. Sheria mpya ya uwekezaji namba 10 ya mwaka 2022 imewavuta wawekezaji wa ndani wakisema imetoa ahueni kwenye kiwango cha kujiandikisha kwa asilimia 50.

Sheria hiyo imepunguza kiwango kwa wawekezaji wa ndani kujiandikisha katika Kituo cha uwekezaji nchini (TIC) ili kufanya biashara kutoka Dola 100,000 hadi Dola 50,000.

Wakizungumza katika maadhimisho ya Nane nane kanda ya magharibi yanayofanyika viwanja vya Ipuli mjini Tabora wafanyabiashara wameeleza kuwa sheria hiyo inawapa ahueni kubwa na wanaona ipo kwa manufaa yao.

Mfanyabiashara Violet Lusana amesema yeye anaifurahia kwani kiwango cha Sh100 milioni kwa wawekezaji wa ndani wanakimudu tofauti na zamani ambao wafanyabiashara walikuwa wanapaswa kuwa na Sh200 milioni.

"Kiwango cha zamani kilikuwa ni kikubwa kwa wawekezaji wa ndani lakini kwa kiwango kipya kwa mujibu wa sheria hiyo kwa kweli tunakimudu,"amesema

Mfanyabiashara Alex Saimon, mkazi wa Chemchem amesema anaagiza bidhaa nje kutokana na sheria hiyo kuwapunguzia makali hivyo kuweka mazingira mazuri ya biashara.

Meneja Kanda ya kati TIC, Venance Mashiba amekiri wafanyabiashara kufurahia sheria hiyo baada ya kutoa elimu na kuwa wamepata mwitikio mkubwa ingawa hakuwa na takwimu kwa wakati huo.

Amesema kwa kupitia maonesho ya Nane nane wanatoa elimu kuhusu kituo hicho sanjali na Sheria  hiyo namba 10 ya mwaka 2022 ambayo imepunguza kiwango cha kuwa na mradi kutoka Dola 100,000 hadi Dola 50,000

Ameongeza kuwa mbali na Sheria hiyo kupunguza kiwango kwa asilimia 50 lakini pia inatoa fursa kwa mwekezaji kupanua mradi wake tofauti na zamani ambapo hawakuruhusiwa.

"Katika sheria hiyo pia mwekezaji anaruhusiwa kupanua mradi wake tofauti na zamani ambapo alikuwa haruhusiwi,"amesema

Mashiba ameeleza kuwa mwitikio wa wawekezaji wa ndani ni mkubwa sana baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa wakisema ina manufaa kwao tofauti na ile ya zamani ambayo ilikuwa inawabana.

Amewakaribisha watanzania wote wanaotaka kuwekeza kuwa wanapatikana katika ofisi za kanda na katika maonesho hayo wana banda lao hivyo watembelee kufahamu fursa na huduma zinazotolewa.

“Watanzania wasiogope kuwekeza na kuona wageni ndio wanastahili kwani watapewa miongozo mbalimbali, lengo kubwa la Serikali ni kuona wawekezaji wote wa ndani wanawekeza na kupata manufaa yakiwemo mapato na Serikali nayo  kupata mapato ambayo yanatekekeza miradi mbalimbali ya maendeleo,”amesema