Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wafanyabiashara Kariakoo wataka mashine ya EFD iondolewe

Dar es Salaam. Wafanyabiashara katika soko la Kariakoo wamesema matumizi ya mashine ya EFDs inayotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) si njia sahihi ya kukusanya kodi.

 Wamesema njia rahisi ya TRA kukusanya mapato ni kuwabana watumishi wake ambao huchukua kodi na kuweka mfukoni na kuiwasilisha kwenye mamlaka hiyo kodi pungufu.

Akitoa maoni leo Mei 22, 2023 mbele ya kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa ajili ya kusikiliza kero za wafanyabiashara nchi nzima, Lucian Sanga amesema kodi nyingi wanazolipa zinaishia kwenye mifuko ya baadhi ya watumishi wa TRA.

"Ukiona silipi kodi ujue tumegawana na mtu wa TRA, kwenye risiti wanasema tunaandika bei pungufu kwasababu tayari bandarini walishusha thamani, ukilipia kodi Sh5 milioni  huwezi kuja kulipia Sh90 milioni,"amesema.

Kwa upande wake mfanyabiashara Renatus Mlelwa amesema mashine ya EFD haiwezi kufanya vizuri kwa wafanyabiashara kwasababu tayari bandarini hakuna usimamizi mzuri wa kodi.

Wafanyabiashara hao wamesema ni muhimu Serikali iwatoze kodi moja bandarini ili wanapoingia kwenye biashara wasipitie usumbufu wowote.

 Mlelwa amesema wamekuwa wakipitia usumbufu mkubwa wa kodi kutokana na watu wachache TRA wanaojali matumbo yao.

"Kuna kampuni naijua inaleta kontena 40 inalipia kontena 20 alafu zingine inaingiza bure sasa hizi kodi zinazosamehewa ndio inakuja kutuumiza sisi,"amesema.

Naye mfanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina la Beatrice amesema ni muhimu kodi ilipiwe bandarini na mashine ya EFD iondolewe kwa kuwa imekuwa chanzo cha rushwa, uongo na kuua biashara nyingi.

Ameeleza kuwa EFD   ina matatizo kwa kuwa haionyeshi faida wala hasara jambo ambalo kwao ni maumivu.

Amesema endapo watu watakaokwenda jehamu watachaguliwa nchini, wafanyabiashara waliopo Tanzania wataongozo kutokana na kusema uongo ambao umechangiwa na sera zilizopo.