Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wafunguka elimu ya utunzaji wa mazingira

Wadau wafunguka elimu ya utunzaji wa mazingira

Muktasari:

  • Katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka ngumu za plastiki katika mito, maziwa na bahari, mradi wa Flipflop umesema utaendelea kutoa elimu kwa jamii namna bora ya kukabiliana na tatizo hilo.

Dar es Salaam. Katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka ngumu za plastiki katika mito, maziwa na bahari, mradi wa Flipflop umesema utaendelea kutoa elimu kwa jamii namna bora ya kukabiliana na tatizo hilo.

Mratibu wa mradi huo nchini Tanzania, Maliha Sumar, amesema hayo jana Ijumaa Aprili 16, 2021 wakati akitoa elimu ya utunzaji wa mazingira na madhara yanayotokana na utupaji ovyo wa taka hizo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wa Wilaya ya Kinondoni na Ilala.

"Mradi huu umelenga kuelimisha jamii jinsi taka za plastiki zinavyoharibu mazingira yetu ikiwemo viumbe hai na namna ya kukabiliana na uharibifu.”

"Tunatoa elimu hii kwa wanafunzi hawa ili wabadilishe tabia zao, wawe na namna nzuri ya kutunza mazingira kwa kutumia taka za plastiki zilizorejeleshwa kwa sababu tunaamini kundi hili likipata elimu nzuri ni rahisi na wao kuwa mabalozi wa kupambana na uharibifu wa mazingira," amesema.

Msanifu  wa mradi huo, Katharina Elleke amesema jamii haina budi kuzingatia sheria na kufuata taratibu za utunzaji wa mazingira kwa sababu kwa  taka hizo zinaweza kutumika katika matumizi mbalimbali.

"Tuwe na elimu ya mazingira endelevu lakini tukumbushane kwa pamoja kutunza na kuhifadhi vyanzo vyetu vya maji ili viumbe hai walioko baharini na ziwani waweze kuishi," amesema Elleke

Daniella Ezekiel ambaye ni mwalimu wa shule ya Haven of Peace Academy amesema licha ya Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya utupaji wa taka za plastiki katika vyanzo vya maji, bado juhudi za pamoja zinahitajika baina ya Serikali, wadau na wananchi kukabiliana na tatizo hilo.

Happiness Mulokozi ni mwalimu wa  Shule ya Msingi Umoja iliyopo Bonyokwa, amesema jamii inao wajibu mkubwa wa kutunza mazingira.

"Hapa tumefundishwa kuwa taka za plastiki zinaweza kurejeleshwa na kutumika katika matumizi mengine kama tulivyonyeshwa hapa boti ya Flipflop iliyotengenezwa na taka za plastiki zilizookotwa katika bahari ya Hindi na ziwa Victoria" amesema.

Glory Boniphace mwanafunzi wa Shule ya Umoja amesema kupitia elimu waliyopewa, atakuwa balozi nzuri kwa wanafunzi wenzake kwa kuwaelekeza madhara ya utupaji holela wa taka za plastiki na athari zake katika mazingira.

Boti hiyo ilitengenezwa mwaka 2017 eneo la Lamu, Kenya na mwaka 2018 ilizinduliwa rasmi Kisumu na sasa inazunguka katika nchini za Kenya, Tanzania na Uganda kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa athari za uchafuzi wa mazingira majini na namna ya kudhibiti taka za plastiki zisiingie katika vyanzo vya maji.

Mradi wa Flipflop unajihusisha na utunzaji wa mazingira katika Ziwa Victoria na Bahari ya Hindi.