Wachimba madini wataka mbadala wa zebaki

Muktasari:
Wachimbaji wadogo mkoani Geita waomba kupatiwa kemikali mbadala ili kuondokana na matumizi ya zebaki inayowasababishia madhara ya kiafya na mazingira
Geita. Wachimbaji wadogo mkoani Geita wameiomba Serikali kushawishi taasisi za tafiti kufanya utafiti ili kupata kemikali itakayotumika badala ya zebaki ili kuondokana na madhara yanayosababishwa na kemikali hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kufunga maonyesho ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Kalangalala mjini Geita, leo Septemba 29, mwenyekiti wa wachimbaji wadogo, Christopher Kadeo amesema baada ya Bunge kupitisha sheria ya kuzuia matumizi ya zebaki, wachimbaji wadogo hawana kemikali mbadala ya kuchenjua dhahabu.
Amesema Bunge la Tanzania katika kikao kilichopita limetia saini ya ukomo wa matumizi ya zebaki ifikapo 2024 lakini wachimbaji wadogo hawana kemikali mbadala itakayowawezesha kuendelea na shughuli za uchenjuaji dhahabu.
Amesema kabla ya zuio la matumizi ya zebaki ni vyema tafiti zikafanyika za kupata kemikali mbadala itakayowasaidia ili kuondokana na madhara yatokanayo na kemikali ya zebaki
Aidha Kadeo ameiomba Serikali kutoa eneo la magema linalomilikiwa na kampuni ya GGM kwa wachimbaji wadogo ili nao wawe na maeneo ya kuchimba na kujipatia kipato.
Akizungumza katika hafla hiyo, Laurensia Bukwimba, mbunge wa jimbo la Busanda amelilalamikia jeshi la polisi kwa kuwabugudhi wachimbaji wadogo wanaobeba dhahabu kupeleka kwenye masoko kwa kuwabambikia kesi na kudai wanahujumu uchumi