Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachaga, Wapare, Wamasai waitwa kutangaza utamaduni, vivutio vya K’njaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu  akizungumza kuhusiana na Tamasha la Mangi Migration festival

Muktasari:

  • Tamasha la Mangi Migration Festival linalotarajiwa kufanyika Desemba 22, 2024 katika viwanja vya Mashujaa Moshi, litajumuisha ngoma za utamaduni, vyakula vya asili na lugha za makabila yaliyopo mkoani Kilimanjaro.

Moshi. Katika kudumisha mila na tamaduni za makabila yaliyopo Mkoa wa Kilimanjaro, Mkoa huo umeandaa tamasha la utamaduni litakaloyakutanisha makabila asili ya mkoa huo,  linalolenga kuchochea ukuaji wa utalii na kuimarisha uchumi.

Tamasha hilo lililopewa jina la Mangi Migration Festival ambalo linatarajiwa kufanyika Desemba 22, 2024 katika viwanja vya Mashujaa, litajumuisha ngoma za utamaduni, vyakula vya asili na lugha za makabila yaliyopo mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 12, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema tamasha hilo litawakutanisha Wachaga, Wapare na wamasai ambao ni makabila ya Mkoa huo na watapata fursa ya kujifunza kupika na kuandaa vyakula vya asili vya makabila hayo, ngoma za utamaduni na lugha za kwao.

"Mkoa wetu wa Kilimanjaro mwezi Desemba tuna matukio mengi na tunapokea wageni wengi na mwaka huu tumekuja na tukio lingine ambalo wananchi watalifurahia la kuonyesha makabila mbalimbali yaliyopo Kilimanjaro wakiwepo Wachaga, Wapare na Wamasai, makabila haya yatakuwa kivutio kikubwa siku hiyo" amesema Babu.

Amesema, "Katika Tamasha hilo tutashuhudia lugha za makabila hayo, ngoma mbalimbali za utamaduni zitaonyeshwa na uwepo wa vyakula mbali vya asili vitapikwa eneo hilo pamoja na nyama choma, nitumie fursa hii kuwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo jirani, kuja kushuhudia tamasha hili la kipekee."

Dayana Msacky ambaye ni muandaaji wa tamasha hilo, amesema dhumuni la Tamasha la Mangi migration Festival ni kuutambulisha utamaduni wa makabila yaliyopo Kilimanjaro pamoja na kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo ili kuvutia watu wengi zaidi kuvitembelea na kuchochea ukuaji wa utalii.

"Katika tamasha hilo, watu watajua vyakula vya asili vya Wachaga, Wapare na Wamasai, lugha yao, viongozi wao wa kimila wanavyooatikana na ni vipi vinywaji vyao vya asili" amesema Msacky na kuongeza;

"Pia tutaonyesha vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Kilimanjaro kwani mbali na mlima Kilimanjaro, yapo maporomoko ya maji maeneo mbalimbali, misitu ya asili, hifadhi ya wanyama pori na vingine vingi, ili kuvutia watu mbalimbali kuvitembelea."

Deogratius Lawrance amesema siku hiyo ya tamasha pia mbali na kuunga harakati za utamaduni na mila za Mkoa wa Kilimanjaro pia kutakuwa na kampeni ya kumkomboa kijana ambapo watapata elimu ya afya na kupata fursa ya kutambua afya zao.

"Siku hiyo tutaona maisha ya watu wa makabila ya Kilimanjaro, lakini pia tutakuwa na harakati za kumkomboa kijana na watapata fursa ya kutambua afya zao kupitia mradi wa Jipevema.