Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wabunge Rukwa washauri maboresho Bandari ya Kasanga

Rukwa. Wakati Bandari ya Kasanga, Mkoa wa Rukwa ikiendelea kuboreshwa, baadhi ya wabunge mkoani humo wameiomba Serikali kushirikiana kati yake na sekta binafsi ili maboresho hayo yawe na tija kiuchumi na nchi za DR Congo, Zambia na Burundi.

Maboresho yanafanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa fedha za ndani huku mamlaka nayo ikibainisha changamoto zinazozikabili zinazohitaji ufumbuzi.

Wabunge hao, Josephat Kandege wa Kalambo na Bupe Mwakang'ata wa viti maalum walifikisha ombi hilo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo alipofika kukagua maendeleo ya bandari hiyo.

Chongolo na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya chama hicho, Issa Ussi Gavu wako mkoani Rukwa kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020/25, uhai wa chama na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Walianza Oktoba 8, 2023 hadi leo Jumatano watakapohitimisha ziara hiyo wakitokea mkoani Katavi. Mkutano huo unafanyikia Sumbawanga Mjini na kuhudhuriwa na mawaziri ama naibu mawaziri kadhaa.

Kadenge alisema kama Taifa tunataka kuboresha kupitia bandari hiyo bila kupitia Zambia kwenye mpaka wa Tunduma, Songwe ni kuwa na meli kubwa ya kuvusha malori ya mizigo hapa

"Njia iliyorahisi kabisa ya kwenda DRC na Zambia ni kuwa na kivuko kikubwa hapa cha kupitisha malori na tukitumia PPP hii inawezekana. Tutaimarisha usafirishaji na kufungua fursa za kiuchumia ili kuvuna utajiri wa DRC ni hii bandari," alisema Kandege

Alisema kuvusha malori yenye mizigo kupitia Kisanga ni rahisi zaidi kwa umbali na gharama hivyo maboresho yakiongezwa yatafungua fursa hiyo kwa mkoa wa Rukwa lakini kupunguza adha ya mrundikano wa malori Tunduma.


Kandege aliungwa mkono na Bupe aliyesema Serikali inapaswa kuwekeza zaidi ili bandari hiyo kuwa na tija ikiwemo hata kutumia PPP.

"Serikali lazima iwekeze, kama ilivyowekeza ila sasa iongeze fedha, kulikuwa na meli mbili ikiwemo ya Liemba, ila sasa hakuna hata moja inayofanya kazi na kusababisha usumbufu kwa wananchi," alisema Bupe

"Tunapaswa kuwe na meli kubwa ambazo zinapishana, hii inakwenda na nyingine inarudi, hili tunaweza ikiwa Serikali itatumia PPP kutakuwa na faida, kwanza Serikali haitatumia fedha zake ila itaongeza tija kwani mwekezaji atatumia fedha zake lakini Serikali nayo itapata mapato," alisema

Bupe alisema changamoto iliyopo Tunduma kwa ule msongamano wa malori tunaweza kuimaliza kwa kutumia bandari hii.

Mbunge huyo alisema Serikali inapaswa kulichukulia hilo kwa uzito ikiwemo kuwa na meli hata za kubeba mizigo kwani kwa sasa hakuna meli hata moja hali inayosababisha adha kwa wananchi.

Akijibu maombi hayo, Chongolo alisema tukipata meli ya mizigo kwenda Congo na kuja hapa kutakuwa na fursa nyingi, haitakuwa mizigo ya saruji pekee na maendeleo yatakuwepo.

"Kulikuwa na meli  ya Liemba na Mwongozo na zote zimesimama. Juzi nimezungumza na waziri wa uchukuzi (Profesa Makame Mbarawa) kuhakikisha wanachukua hatua za haraka ili meli moja ianze kazi na hii ni meli ya Mwongozo imepandishwa kwenye chelezo kwa ukaguzi na Desemba itashushwa kwenye maji na kuanza kazi," alisema

Kuhusu meli ya Liemba iliyotengenezwa miaka 100 nyuma, fedha zimetengwa kwa ajili ya maboresho makubwa.

Chongolo alisema Serikali imefanya uamuzi wa kuboresha bandari kubwa na ndogo nchini na mwezi huu kuna mkataba unasainiwa Kigoma wa kujenga kanakana na ujenzi wa meli utafuata.

"Lengo ni kujenga meli kubwa ya mizigo zaidi ya tani 3,000 ambayo ni sawa na malori 30 na muda mfupi tutaondokana na changamoto ya kule Tunduma. Leo tunaongea kama hadithi lakini ipo siku mtatuelewa na tunataka kuona miaka michache ijayo njia ya Matai- Sumbawanga inakuwa njia kuu ya usafirishaji," alisema

Awali, Ofisi wa Bandari, Rodriues Valentin akisoma taarifa mbele ya Chongolo na ujumbe wake alisema maboresho mbalimbali katika bandari hiyo ndogo  yanaendelea ikiwemo kufunga mashine za kupakia na kushusha mizigo.

Alisema katika mwaka wa fedha 2021/22 bandari hiyo ilihudumia meli 34 na mwaka 2022/23 meli 32. Kuanzia Julai mwaka huu hadi Oktoba 23 wamehudumia meli moja pekee.

Valentin alibainisha changamoto zinazowakabili ikiwemo ya kufunguliwa kwa kiwanda cha saruji cha Kibimba huku DR Congo kimeongeza ushindani wa kibiashara kwa wateja wa Congo waliokuwa wanatumia bandari hiyo.

Alisema bandari hiyo ilijengwa kuanzia 1995 hadi 1998 na awamu ya pili 2018 hadi mwaka huu ikihudumia nchi za Burundi, Zambia na DR Congo ikiwa na gati lenye urefu wa mita 120 na wastani wa kina cha maji mita 14.