Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vurugu zazuka uchaguzi Chadema Kanda ya Nyasa

Wafuasi wa Chadema Kanda ya Nyasa wakiwa katika purukushani mlangoni  katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikra Maria wa Neema katika mji wa Makambako. Picha na Saddam Sadick

Njombe. Ikiwa inaelekea uchaguzi wa kuwapata Mwenyekiti, Makamu na Mweka Hazina wa Chadema Kanda ya Nyasa, vurugu zimeibuka na kusababisha mvutano baina ya makada wa chama hicho.

Hata hivyo, haikufahamika haraka chanzo cha vurugu hizo, ambapo wakati wajumbe wa mkutano mkuu wakiendelea kuingia ukumbini, ghafla baadhi ya waliokuwa wametangulia walirejea tena getini wakitishia kususia uchaguzi.

Waandishi wa habari hawajaruhusiwa kuingia ndani ya geti wala ukumbini wakielekezwa eneo maalumu la kukaa kusubiri wagombea watakapoingia ndani ndio wataruhusiwa kwa dakika kadhaa.

Walinzi wa chama hicho walikuwa makini kuingilia kati vurugu hizo, huku baadhi wakielekezwa kuwaondoa wanaotishia kususia uchaguzi huo.

Licha ya kutokea vurugu hizo, amani imerejea hadi sasa wajumbe wanaendelea kuhakikiwa kwa ajili ya kuingia ukumbini kusubiri hatua ya uchaguzi kuwapata viongozi wa Kanda.