Vodacom, Britam wazindua mauzo ya bima ya magari kwa simu
Muktasari:
- Kampuni hizo zimeweka huduma hiyo ili kuwarahisishia watumiaji uwezekano wa kupata huduma hiyo.
Dar es Salaam. Huduma za bima zimeendelea kurahisishwa, ambapo sasa huduma hiyo inapatikana kupitia simu za mkononi.
Leo Aprili 12, 2021 kampuni ya huduma za simu ya Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Britam wamezindua huduma mpya ya vodabima ambapo sasa watumiaji wa mtandao wa Vodacom wataweza kakata na kulipia bima kwa kutumia simu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mpesa Epimack Mbeteni amesema kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya bima nchi Vodacom na Britam wameunga kutoa huduma za bima kwa urahisi zaidi kupitia simu za mkononi.
"Kwa sasa tutaanza na bima ya magari ile ndogo (3rd Party) baadaye tutahamia bima nyingine, uzuri wa huduma hii unaweza kununua ukiwa popote kwa kutumia M-pesa na unaweza kumnunulia yeyote muda wowote," amesema Mbeteni.
Afisa mtendaji Mkuu wa Britam Raymond Komanga yeye amesema ushirika huo na Vodacom utawaongezea wateja na kuongeza umiliki wao wa soko hadi kufikia asilimia 8 kutoka asilimia 5 waliyonayo sasa.
"Hatua hii itaongeza upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi kwa urahisi. Kwetu itatuongezea wateja na biashara, kwa sasa tulikuwa tunashika namba 6 soko lakini ndani ya mwaka mmoja huenda tukafika hadi nafasi ya 4," amesema