Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vituo vinane vya Tehama kujengwa Tanzania

Muktasari:

  • Tume ya Tehama (ICTC) imewaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaoendelea mkoa wa Lindi kuwa Serikali inatarajia kujenga vituo vinane vya ubunifu wa teknolojia.

Lindi. Serikali ya Tanzania inatarajia kujenga vituo vinane nchini vya ubunifu wa teknolojia vitakayowezesha wananchi kuvitumia kuboresha kazi zao za kibunifu.

Hayo yamesemwa leo Jumanne, Novemba 14, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama (ICTC), Dk Nkundwe Mwasaga wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyikia Uwanja wa Ilulu, Mkoa wa Lindi.

Dk Mwasaga amesema vituo hivyo vinatarajiwa kujengwa mikoa ya Dodoma, Tanga, Lindi, Mbeya, Dar es Salaam, Arusha pamoja na Zanzibar.

Ujenzi wa vituo hivyo ni sehemu ya vipaumbele 13 vya ICTC ambavyo vina lengo la kuleta mapinduzi ya teknolojia na ubunifu nchini.

Amesema huo ni mpango wa awali: "lakini mkakati uliopo ni kujenga vituo katika mikoa yote na wilaya zote ili wananchi waweze kuvitumia na kujifunza suala zima la teknolojia."

Mkurugenzi huyo amesema vituo hivyo vitajengwa maeneo karibu na vyuo na shule ambavyo vitasaidia vijana nchini kubuni na kuanzisha kampuni changa za ubunifu wa vitu mbalimbali vinavyuhusiana na teknolojia.

Pia, vitatumika kuendeleza bunifu zao na vitakuwa na uwezo wa kuingiza watu zaidi ya 200 kwa wakati mmoja.

Dk Mwasaga amesema, watu wengi wamekuwa na hofu na akili bandia au akili mnemba (Artificial Intelligence – AI) kwamba inaweza kuwakosesha kazi, jambo ambalo siyo kweli, kwani akili bandia inaleta tija na watu wakipewa ujuzi mpya kuhusu teknolojia hiyo itasaidia.

Amesema watajenga kituo cha Artificial Intelligence kwa ajili ya kuendeleza wataalam wa Tehama pamoja na kuwezesha mafunzo maalum ya wataalam wa Tehama 500 ili kukuza na kuendeleza ujuzi wa Tehama nchini.

“Tunatarajia kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya Tehama (ICT Refurbishment and Assembly Centre) na vituo vya majaribio vya ubunifu Tehama (District ICT Startups Innovation Hubs) katika wilaya 10,” amesema Dk Mwasaga

Amesema watafanya tafiti za maendeleo ya Tehama nchini na kufanya tathmini ya kitaifa ya hatua za utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya Tehama.

Amesema wataratibu na kuandaa matukio ya kuvutia uwekezaji na kutangaza masoko ya bidhaa za Tehama ndani na nje ya nchi.

“Tutashirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za Tehama ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za Tehama hapa nchini,” amesema

Alisema, majukumu mengine watakayoyafanya ni pamoja na kukuza soko la bidhaa na huduma za kampuni ndogondogo “startup” kwa kushiriki maonesho na makongamano yanayohusu fursa za startups duniani.

Pia, ICTC inakusudia kuratibu na kutengeneza mfumo wa usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Tehama na kufanya tafiti za kuweza kufanya maboresho ya sera kulingana na mabadiliko ya teknolojia.

Ametaja mikakati mingine ni kujenga Metaverse Studio kwa ajili ya kutengeneza maudhui ya metaverse na pia kuboresha maudhui ya mitandao ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti za maendeleo ya Tehama kwa kila wilaya na kuanzisha Kituo cha Resilience Academy hapa nchini.