Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi wa dini wataja faida nne bwawa la Nyerere

Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri wa Nishati Januari Makamba, pale walipotembelea bwawa la kufua umeme la Mwl Nyerere

Muktasari:

  • CPCT watembelea mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP), waeleza faida zake endapo utaanza kufanya kazi ifika Juni mwakani

Pwani. Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), limesema mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakuwa na manufaa makubwa manne ambayo ni kufua umeme, uvuvi, utalii na ufugaji.

Kauli hiyo wameitoa leo Alhamisi, Julai 13, 2023 wakati wanazungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mradi mradi huo utakaogharimu Sh6.5 trilioni ambao utaanza majaribio ya uzalishaji Februari mwakani huku uzalishaji kamili ukitarajiwa kuanza Juni 2024.

Mmoja wa waasisi wa CPCT, Askofu Slyvester Gamanywa, amesema Watanzania watakuwa na uhakika wa umeme mradi ukikamilika, lakini pia watapata fursa za kilimo, uvuvi na utalii ambazo zitawaongezea kipato kwa namna moja au nyingine.

Amesema mradi wa JNHPP ni salama kwa maendeleo ya Taifa kwa kuwa wametembelea na wamepata maelezo ya kutosha kutoka kwa wataalamu mbalimbali hivyo Watanzania wana kila sababu ya kujivunia mradi huo.

“Nawahakikishia wananchi kama yalikuwapo majungu kuhusu mradi basi niwaambia CPCT imejiridhisha salama na una faida kubwa kwa Watanzania na uchumi wa Taifa. Nichukue fursa hii kuwaambia Watanzania kwamba mradi huu ukikamilika Tanzania itaandika historia nyingine,” amesema Gamanywa.

“CPCT tulikuwa tunasikia tu, kuhusu mradi huu, lakini leo tumeona kazi kubwa imefanyika katika umalizaji wa mradi ulioanzishwa na Serikali ya awamu ya tano. Ukitembelea mradi huu utajionea mambo mengi, tuishukuru Serikali kuweka utaratibu wa viongozi wa dini kuja,” amesema Gamanywa.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CPCT, Askofu Daniel Awet ameishauri Serikali kuweka utaratibu wa kufanya ukarabati wa mitambo ya mradi huo kwa wakati ili kuwepo na tija zaidi.

Amefafanua kuwa mradi wa JNHPP umetumia fedha nyingi, endapo hautakarabatiwa kama ilivyopangwa itakuwa hasara kwa Taifa itakayo sababisha shughuli kusimama.

Pia askofu Awet ameiomba Serikali kutumia wataalamu wazawa katika kuhakikisha wanautunza mradi huo.

“CPCT tumetembelea na kuona maendeleo ya mradi huu, tutakwenda kuwaeleza waumini kuhusu umuhimu wake, lakini tunaomba Serikali itoe elimu inapoanzisha mradi maana wapinzani hawakosi.

Amesisitiza kuwa JNHPP ni mradi mkubwa wa kitaifa wenye manufaa makubwa kwa maendeleo ya Taifa, huku akiipongeza Serikali kupitia Wizara ya Nishati, kwa usimamizi bora hadi hatua iliyofikiwa ya asilimia takribani 90.

Naye Waziri wa Nishati, January Makamba amesema moja ya faida za mradi huo ni ujenzi wa daraja jingine kubwa katika Mto Rufiji ambalo limeshakamilika, akisema kwa siku zijazo wananchi wanaotoka mikoa ya kusini kwenda Dodoma hawatalazimika kupitia Dar es Salaam badala yake watakatiza katika mradi huo hadi Chalinze.

“Mradi huu una faida katika sekta ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa barabara itakayoanzia maeneo Utete mkoani Pwani ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa mikoa ya kusini na Pwani. Pia mradi wa JNHPP utakuwa manufaa kwa sekta za maji kwa kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa urahisi,” amesema Waziri Makamba.

Waziri Makamba amesema Serikali pia inatekeleza miradi mingine ya kufua umeme ukiwamo wa Rusumo unaojumuisha Tanzania, Rwanda na Burundi ambao ujenzi wake upo mbioni kukamilika.