Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijiji Ruangwa kunufaika na mradi wa maji Lindi

Muktasari:

  • Ni wakazi wa vijiji kadhaa watakaonufaika na mradi wa maji   ambao utagharimu kiasi cha Sh119 bilioni, unaojengwa katika Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Lindi. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainabu Telack amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji, kwa kuacha kukata miti ovyo pamoja na kwenda kunywesha mifugo kwenye vyanzo vya maji.

Akizungumza leo kwenye ziara yake ya  siku moja alipokwenda kutembelea mradi wa maji, unaojengwa katika Kijiji cha Chimbila B, Wiliya ya Ruangwa mkoani Lindi, Telack amesema kuwa wananchi waache tabia ya kuharibu vyanzo vya maji, kwa kukata miti hovyo na kwenda kunywesha mifugo.

"Nitoe wito kwa wananchi wa Lindi, waache tabia ya kukata miti ovyo, pamoja na kwenda kupeleka mifugo kwenye vyanzo vya maji. Sasa hivi mnaona maji mengi kutokana na mvua zinazonyesha lakini mvua zikimalizika mtaona adha yake, tutunze mazingira, nilishasema wenye mifugo waende wakachimbe malambo, siyo kupeleka kwenye vyanzo vya maji," amesema Telack.

Katika hatua nyingine, Telack amemtaka Mkandarasi  wa mradi kupitia Mamkala ya  Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) kuhakikisha wanamaliza mradi huo kwa wakati, ili wananchi wapate maji yaliyosafi na salama.

"Maji wanayotumia sasa hivi yana chumvi nyingi, niwaombe wasimamizi wa mradi, akiwemo na meneja wa mradi mjitahidi kuhakikisha mradi unamalizika kwa wakati ili wananchi waweze kupata maji yalio salama zaidi," amesema.

Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa), Mhandisi Muhibu Rubasa amesema kuwa mradi huo  unatoa maji kutoka Mto Nyangao utahudumia vijiji 56, ambapo Lindi itakuwa kijiji kimoja, Nachingwea vijiji 21 pamoja na vijiji 34 vya Wilaya ya Ruangwa.

Mhandisi Rubasa amefafanua kuwa, mradi huo wa maji utagharimu kiasi cha Sh119 bilioni, ambapo hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 11 na unatarajiwa kumalizika 2025.

"Mradi huu utakapokamilika, utahudumia vijiji 56, wakazi zaidi ya 1,000 na malengo ya mradi huu kumalizika hadi ifikapo 2025 na hadi sasa mkandarasi amefikia asilimia 11 ya mradi," amesema Rubasa.

Naye ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chimbila B, Stella Victor amesema mradi utakapokamilika utawasaidia wananchi wa Ruangwa na maeneo mengine, kwani kwa sasa maji wanayotumia yana chumvi.

"Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutuona na kutuletea mradi mkubwa wa maji kwani utakapomalizika utaondoa adha ya maji iliyopo sasa, kwa wananchi wa Ruangwa na maeneo mengine,” amesema Stella.