Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana 96,894 wanufaika mafunzo ya ujuzi Veta

Muktasari:

Jumla ya vijana 96,894 wamepatiwa mafunzo ya ujuzi nchini kati ya mwaka 2016/17 kupitia vyuo vya Veta.


Dodoma. Jumla ya vijana 96,894 wamepatiwa mafunzo ya ujuzi nchini kati ya mwaka 2016/17 kupitia vyuo vya Veta.

Naibu Waziri Ofisi Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ameliambia Bunge leo Jumatano Aprili 19, 2023.

Katambi alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli (CCM) ambaye ametaka kujua ni Watanzania wangapi wamejitokeza kupata fursa ya mafunzo maalumu ya ujuzi yaliyotangazwa kupitia Veta kote nchini.

Naibu Waziri amesema katika kipindi hicho, vijana 215,233 waliojitokeza kuomba mafunzo hayo kupitia vyuo vya Veta na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC).

“Kati ya idadi ya waliopata mafunzo hayo, vijana 74,598 wamepatiwa mafunzo kwa njia ya uanagenzi na vijana 22,296 wamepatiwa mafunzo kupitia njia ya urasimishaji ujuzi (RPL),” amesema Katambi.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwajali vijana na kuwapatia fursa kila zinapojitokeza ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kujitegemea.