Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana 500 Malinyi kuondokana na hali ya utegemezi

Mratibu wa Mtandao wa Wakulima na Wafugaji Morogoro (MVIWAMORO), Joseph Sengasenga

Malinyi. Vijana zaidi ya 500 wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro wanatarajia kuondokana na hali ya utegemezi baada ya kujengewa uwezo katika stadi mbalimbali ikiwemo za ufundi, lengo likiwa ni kuwawezesha kujipatia kipato kupitia ujuzi watakaoupata ili waweze kujiajiri.

Mratibu wa Mtandao wa vikundi vya Wakulima na Wafugaji Morogoro (Mviwamoro) ambao ni waandaaji wa tamasha la Kaa Kijanja, Ufundi Stadi Ajira kwa Vijana, Joseph Sengasenga amesema hayo Oktoba 2, 2023 wakati wa tamasha hilo lililolenga kuhamasisha vijana kutumia ujuzi na vipaji walivyonavyo kujiajiri lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Sofi Majiji.

Sengasenga amesema ujuzi huo wa vijana utatengeneza ajira kupitia elimu ya ufundi stadi na kilimo na kwamba Mviwamoro kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania ambao ndio wafadhili wa tamasha hilo wanatambua kuwa matamasha ya aina hiyo yatawawezesha vijana kujitambua na kuacha kuwa tegemezi.

Amesema tamasha linahamashisha vijana waliopo nje ya mradi wa SET ambapo vijana hao 500 waliweza kujengewa uwezo hasa katika ufundi stadi na imekuwa ni nafasi ya kipekee kuwafanya walioko nje ambao hawajapata mafunzo kuamini kuwa ufundi stadi ni moja ya ajira.

“Sisi kama Mviwamoro tuna imani kwamba ufundi stadi wowote unahitaji kuwa na mtaji na uzalishaji na vijana hawa wanahitaji kuwa na soko la uhakika ndio maana tumefanya kuwaonyesha ni kwa namna gani ufundi ndio njia pekee ya mafanikio kwa kujipatia kipato na kuweza kutatua changamoto mbalimbali hasa katika familia zao,” amesema

“Utaenda katika maeneo mbalimbali hasa katika kilimo kwenye mnyororo mzima wa thamani, pia tumeangalia katika ufundi, ufugaji kwa kuhakikisha vijana wanajengewa ujuzi na wanachokifanya kinakuwa na tija,” amesema

Aidha amesema wametumia tamasha kama njia pekee ya kuwafikia kwa wingi na kufikisha ujumbe ambayo itawasaidia vijana ili kuongeza hamasa.

Maelfu ya vijana kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Malinyi wamejitokeza kushuhudia michezo mbalimbali kwenye tamasha hilo ikiwemo mpira wa Miguu, ukunaji wa nazi, riadha (kukimbia), pamoja na michezo ingine ya kiutamaduni.

Kijana mkazi wa kata ya Itete Blandina Shirima amesema yeye kama kijana ameweza kupata fursa na kunufaika kupitia mradi wa Set kwa kupata mafunzo ya kilimo biashara ambapo kimemfumbua kama kijana kwa kumpa mawazo chanja kwani mwanzo alifiki kilimo ni cha watu wa hali ya chini kumbe ni cha watu wote kwani kinakuwezesha kuzalisha na kunufaisha familia.

“Thamani ya kilimo niliyoiona inaweza kukuza uchumi wa taifa kwa kununua pembejeo ikiwa ni pamoja na kulima kilimo cha chakula na kuyafanyia biashara na kuwanufaisha watanzania,”amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sebastian Walyuba amesema mradi huo umetengeneza matarajio ya mafanikio ya mbele kwa vijana kujiandaa kuwa na ufundi stadi kwa maisha yao na katika shughuli zao za kila siku, ambapo aliwahimiza kuwa wabunifu ili kuweza kuongeza uchumi, kipato cha kaya na taifa kwa ujumla.

Mtaalamu wa vijana kutoka SwissContact kwenye mradi wa Skills for Employment Tanzania(SET) Paul Mideye amesema mradi huo unalenga vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ili waweze kujitegemea baada ya kujengewa uwezo katika ufundi stadi hasa katika kilimo.

Mkazi wa kijiji cha Sofi Majiji, Najim Gwawa ambaye ni mnufaika wa mradi amesema kupitia mradi huo umeweza kuwasaidia vijana kutoilaumu Serikali juu ya suala la ajira kwamba aiajiri kumbe kupitia taasisi binafsi zinasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza malalamiko na tatizo la ajira kwa kuwezesha vijana kupata ujuzi na kujiajiri.

“Maisha kidogo yalikuwa changamoto kwani ukiishi bila ujuzi unatafsirika kuwa unafanya shughuli gani lakini baada ya mafunzo tumeona namna gani unaweza kutafuta mtaji wako na kujisimamia tulifundishwa zaidi masuala ya uchumi, imetupunguzia zaidi ile kuisumbua jamii,” amesema.

Tamasha hilo ni muendelezo wa miradi miwili ya Skills for Employment Tanzania (SET) na Opportunity for Youth Employment (OYE) inayofadhiliwa na serikali ya Uswisi ambapo vijana zaidi ya 1,600 kutoka halmashauri za wilaya za Malinyi, Mvomero, Kilombero, Gairo, Manispaa ya Morogoro na Kilosa wanatarajia kunufaika na miradi hiyo ikiwa na nia ya kuwawezesha kujiajiri.