Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Manara aibukia kwa Diamond, amwambia kura za Tandale zote zake

Muktasari:

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameamsha popo katika tamasha la kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa mwanamuziki Diamond Platnumz baada ya kuingiza siasa

Dar es Salaam. Kuna usemi usemao ‘kwenye sherehe tingatinga limefikaje’ ndivyo unavyoweza kusema baada ya msemaji wa klabu wa Simba, Haji Manara kuingiza siasa kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa mwanamuziki Diamond.

Haji Manara aliufananisha umati uliofika kumuona nyota huyo na wapiga kura kwa kusema Diamond angepita bila kupingwa iwapo angegombea nafasi yoyote ya ubunge.

“Kama Diamond angetaka kufanya siasa hizi zote kura zake nawaambia, nimejaribu kumuuliza kuhusu hilo lakini mwenyewe amesema hataki kufanya siasa hivyo wanasiasa mtulize roho zenu,” amesema Manara.

Mara baada ya kusema hayo shangwe ziliibuka uwanjani hapo na baadaye Manara alizungumza tena na baadaye alitoa mipira kwa shule za Tandale.

Amesema ili watoto wakue vizuri ni muhimu wapate muda wa kucheza hivyo anatoa mipira hiyo ili kuhakikisha wanashiriki michezo.

Amesema katika kumuunga mkono Diamond amezungumza na wadau ambao wamekubali kuweka ligi Tandale itakayofahamika kwa jina la ‘Diamond Tandale Super Cup.’

Manara ametangaza kugharamia ada za wanafunzi wote walemavu watakaoanza shule Januari mwakani.

“Wanafunzi walemavu wote watakaoanza mwakani nitalipa ada kuanzia msingi hadi sekondari ili mradi iwe shule za serikali,” amesema Manara huku akishangiliwa.