Uzinduzi kitabu cha mzee Mwinyi wawakutanisha viongozi

Muktasari:
- Uzinduzi wa kitabu cha maisha binafsi ya Rais mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi umewakutanisha viongozi wastaafu na waliopo madarakani.
Dar es Salaam. Uzinduzi wa kitabu cha maisha binafsi ya Rais mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi umewakutanisha viongozi wastaafu na waliopo madarakani.
Uzinduzi huo unafanyika leo Jumamosi Mei 8, 2021 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ndio mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Viongozi wa dini, waandishi wa habari, mabalozi, viongozi wastaafu, waliopo madarakani ni kati ya waliohudhuria uzinduzi wa kitabu hicho.
Baadhi ya waliohudhuria ni Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.
Wengine ni Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Mwinyi amezaliwa Mei 8, 1925 na uzinduzi huo unafanyika leo siku ambayo kiongozi huyo mstaafu anasherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 96.