Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uwindaji wa kitalii waleta neema nchini

New Content Item (1)

Uwindaji wa Kitalii Wanufaisha Nchi kwa zaidi ya sh 9.6  Billioni zatolewa Kwa Halmashauri na Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu - Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi.

Morogoro. Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa) Mabula Misungwi, amesema shughuli za Uwindaji wa Kitalii zinazofanywa katika mapori ya akiba na  tengefu nchini, zina manufaa na mchango katika kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa na Kamishna Misungwi Mei 11, 2023 (Alhamis) katika Ofisi za Pori la Akiba Kizigo lililopo Wilaya ya Manyoni mkoani Singida pale alipokuwa akiongea na watumishi wa Pori hilo katika ziara yake ya kikazi Kanda ya Kati.

Bosi huyo mamlaka hiyo, amesema Serikali kupitia Tawa imetoa Sh9.6 billioni kwa Halmashauri na vijiji huku wanufaika wakiwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa mapori ya akiba na yale tengefu nchini na kwamba ni fedha zitokanazo na asilimia 25 ya ada ya Wanyamapori waliowindwa pamoja na Utalii wa picha katika kipindi cha kuanzia Aprili 2022 Mpaka Desemba 2022.

"Niwaeleze tu kuwa manufaa haya ni Jamii, mwananchi mmoja mmoja hususan wale waishio pembezoni mwa mapori ya akiba na mapori tengefu," amesema.

Katika ziara hiyo, Kamishna Misungwi amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo (ujenzi wa visima vya maji safi, nyumba za watumishi na ofisi) ambapo amekutana na kuzungumza na viongozi wa Tawa Kanda ya kati, na watumishi wa pori la akiba Kizigo.

Pamoja na mambo mengine, Kamishna ameupongeza uongozi wa pori hilo na Kanda Kwa ujumla Kwa kazi wanayoifanya. Pia amewataka watumishi hao kuongeza ubunifu, bidii ya kazi ili kuongeza mapato ya malaka na hivyo kuchangia katika pato la Taifa.

"Katika kipindi cha Mwaka huu wa fedha tuhakikishe tunafanya kazi kwa kujituma, kwa bidii ili kurudisha shukrani kwa Serikali kwa namna inavyotujali," amesema Kamishna huyo wa Uhifadhu wa Tawa.

Amewaagiza viongozi na Watumishi wa Kanda ya kati kuhakikisha vitalu vyote vya uwindaji wa kitalii katika Pori la Akiba Kizigo vinapata wawekezaji, hasa ikizingatiwa kuwa pori hilo lina jumla ya vitalu vinne vya uwindaji ambapo viwili kati ya vinne vimepata wawekezaji

Kuhusu wanyamapori wakali na waharibifu, Kamishna Misungwi amesema mkazo wa Wizara na Tawa ni kuhakikisha kuwa adha wanayoipata wananchi kutokana na Wanyamapori Wakali na Waharibifu inadhibitiwa kikamilifu kwa kupambana usiku na mchana.

Pia amesema viongozi wa vijiji, kata na wilaya wataendelea kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria ya matumizi bora ya ardhi kwani wao ndio huwapatia wananchi vibali vya ujenzi na makazi ambapo kwa kutoelewa, wananchi huanzisha kilimo na makazi holela kitu kinachosababisha kuvamiwa Tembo.

Ameelekeza watumishi wa pori hilo kuimarisha ushirikiano na wadau wa uhifadhi (Wildlife Conservation Society), Lakini pia kujenga mahusiano bora kwa kufanya kazi na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo, kitu ambacho kitaleta taswira nzuri ya taasisi.

Awali, Kamanda wa uhifadhi wa pori la akiba Kizigo, Ogossy Gesaya amesema katika kipindi 2022 - 2023 pori hilo limekusanya zaidi ya Sh704 millioni kutokana na shughuli za uwindaji wa kitalii kwa watalii watano (5) na Watazamaji (observers) 14 waliotembelea pori hilo na kuahidi ongezeko kubwa la mapato kwa mwaka ujao wa fedha.

Kuhusu miradi ya maendeleo Kamanda Gesaya amesema katika kipindi cha Mwaka 2020/2022 mpaka 2023 Pori limesimamia jumla ya miradi mitano (5) ambapo minne imeisha kwa asilimia 100 na mmoja uko asilimia 90.

Gesaya amesema baada ya kupatiwa vitendea kazi vya kutosha, hali ya ujangili imepungua kwa kiasi kikubwa mwaka 2022/23, ikilinganishwa na ilivyokuwa Mwaka 2021, pia ushirikiano kati ya pori hilo, wawekezaji na wadau wa uhifadhi (WCS), umeboreka.

Kwa upande mwingine Kamishana Gesaya ameipongeza menejimenti ya Tawa kwa kuboresha maisha ya watumishi kimaslahi na kuwapatia vitendea kazi jambo ambalo limeongeza morali ya kujituma katika kazi.