Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utata ‘kukamatwa’ wakili Madeleka

Muktasari:

  • Licha ya kuwepo taarifa za kukamatwa kwa Wakili Peter Madeleka jijini hapa, wasemaji wa Jeshi la Polisi hawajawa tayari kuzungumzia tukio hilo, huku makundi ya wanaharakati na wanasiasa wakishinikiza haki itendeke.


Dar es Salaam. Licha ya kuwepo taarifa za kukamatwa kwa Wakili Peter Madeleka jijini hapa, wasemaji wa Jeshi la Polisi hawajawa tayari kuzungumzia tukio hilo, huku makundi ya wanaharakati na wanasiasa wakishinikiza haki itendeke.

Juzi msemaji wa jeshi hilo, David Misime alipoulizwa kwa simu alisema hana taarifa hiyo kwa kuwa alikuwa Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Debora Magiligimba alisema suala hilo atafutwe Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ambaye naye simu yake ilipokewa na msaidizi aliyesema bosi wake yuko kikaoni.

Kukamatwa kwa Madeleka kumekuja ikiwa ni siku chache tangu alipotuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akidai kuwepo kwa njama zinazoratibiwa na baadhi ya maofisa wa idara ya uhamiaji (aliowataja majina) kuwa walipanga kumuua. Kabla ya kuibua utata wa taarifa za kukamatwa wakili wa Madeleka, Paul Kisabo alitumia ukurasa wake wa Twitter kueleza maofisa hao walimkamata eneo la kuegesha magari la Hoteli ya Serena ikiwa ni saa chache baada ya kusambaa taarifa za kuchukuliwa na watu wasiojulikana.

Baadaye Kisabo aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa wakili Madeleka alikuwa akihojiwa katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani jijini hapa.

“Nimetoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda huu, tangu 18:00hrs (saa 12 jioni) nilikuwa hapa kutoa legal representation kwa @PMadeleka aliyekamatwa Serena Hotel Dar,” aliandika.

Kwa mujibu wa Kisabo, polisi walifanya upekuzi katika hoteli aliyofikia Madeleka, hata hivyyo hakuruhusiwa kushuhudia upekuzi huo wa mteja wake.

Kisabo jana alieleza changamoto ya kuzuiliwa kumwona Madeleka baada ya kufika Kitengo cha Uhalifu wa Mitandaoni chini ya kanda maalumu ya Dar es Salaam.

Wakili huyo anakamatwa ikiwa ni siku chache baada ya kunukuliwa katika mitandao ya kijamii akituhumu baadhi ya watu kupanga njama za kumteka. Msemaji wa ACT Wazalendo wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarala Maharagande ametoa wito wa kuachiliwa kwa wakili huyo.