Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usambazaji umeme wa Bwawa la Nyerere wanukia  

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Irene Gowelle akizungumza leo Julai 28, 2026 mara baada ya kitembelea mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze kwenda Dodoma uliofikia asilimia 94.

Muktasari:

  • Kukamilika kwa mradi huo utawezesha umeme wote unaozalishwa bwawa la Nyerere kufikia walaji kote nchini.

Pwani. Zaidi ya megawati 2115 za umeme unaozalishwa katika Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), zinatarajiwa kuanza kusambazwa nchini kufuatia kukamilika kwa asilimia 94 mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze kwenda Dodoma.

Kukamilika kwa mradi huo utawezesha umeme wote unaozalishwa Bwawa la Nyerere kufikia walaji kama anavyosema Meneja wa mradi huo, Mhandisi Newton Mwakifwamba.

Mradi huo wenye thamani ya Sh514 bilioni wa kilomita 345 unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania, unahusisha wigo wa upanuzi wa njia na vituo vya kupoza umeme vya Chalinze na Dodoma.

Mhandisi Mwakifwamba amesema hayo leo Jumanne, Julai 28, 2026 wakati wa ziara ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Irene Gowelle kukagua mradi huo.

"Sasa hivi JNHPP ina uwezo wa kuzalisha umeme megawati 2115 lakini zote haziwafikii walaji kwa asilimia 100. Sasa hivi tunasafirisha umeme megawati 850 pekee kutoka kwenye bwawa hilo,”amesema Mwakifwamba.

Akifafanua zaidi amesema bwawa hilo liko tayari lakini njia za kuwapelekea wateja zina uwezo wa kusafirisha megawati 850 hivyo wamejenga njia hiyo ili umeme wote uende kwa wateja.

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Irene Gowelle akizungumza leo Julai 28, 2026 mara baada ya kitembelea mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze kwenda Dodoma uliofikia asilimia 94.

"Sasa tukikamilisha mradi huu zile megawati 2115 zote zitaenda kwa walaji kupitia laini hii ya msongo wa kilovolti 400 kwa asilimia 100, pia utawezesha biashara ya umeme ya nje ya nchi," amefafanua.


Umeme kukatwa

Kwa sasa mkandarasi anatarajiwa kuanza kazi ya kuvuta nyaya za umeme katika eneo la Mkambarani, mkoani Morogoro, hatua inayohitaji kuzimwa kwa muda baadhi ya njia kuu za kusafirisha umeme za kilovolti 220 na 132 ili kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na utekelezaji wa kazi kwa ufanisi.

Mhandisi Mwakifwamba amesema maeneo ya Mkambarani, Kikombo na Nkonze yatakuwa kitovu cha kazi hizo na kwamba, njia mpya za umeme zitaunganishwa sambamba na miundombinu iliyopo ili kukamilisha mradi huo kwa usalama na ufanisi.

"Njia ya kwanza ni Morogoro one, Morogoro two na njia ya tatu ya msongo wa kilovolti 132 inayotoka Chalinze kwenda Morogoro. Eneo hili tukimaliza kazi tutaenda awamu ya pili ya eneo la jeshi la Kikombo.

"Kuna eneo la Mkonze Dodoma pia tutavuka na njia hizi zote tutakuwa tunazima umeme,” amesema Mwakifwamba.

“Tukiwa tunazima umeme kwa ajili ya Kikombo uzimaji huo huo wa umeme utatuwezesha kuvuka eneo la Mkonze, kwa hiyo tutavuka maeneo mawili kwa pamoja ambayo ni Agosti 11 hadi 17, 2026," amesema Mwakifwamba.

"Maandalizi ya kiufundi yamefanyika ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo hautaathiri huduma za usafiri wa treni hiyo."


Maeneo yatakayoathirika

Akiweka wazi maeneo yatakayoathirika, Gowelle ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Tanesco, amesema wateja wa Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Magharibi na Kaskazini Magharibi yote itaathiriwa katika tarehe tofauti.

"Awamu ya kwanza itaanza Julai 30, 2026 hadi Agosti 4, 2026, awamu ya pili itaanza Agosti 11, 2026 hadi 17, 2026. Huduma ya umeme itakuwa inakosekana kuanzia asubuhi saa 12 hadi saa 11 jioni,”amesema.

Gowelle amesema kukatwa kwa umeme katika mikoa hiyo ni kwa ajili ya usalama na kumuwezesha mkandarasi kufanya kazi.

"Mikoa ambayo haitaathirika ni Dar es Salaam, Pwani na mikoa ya Kusini yani Mtwara na Lindi," amesema.

Hata hivyo, Gowelle amesisitiza kuwa hakuna mteja atakayekosa huduma ya umeme kwa siku zote za matengenezo mfululizo, kwa kuwa ratiba ya katizo itatofautiana kulingana na maeneo na maendeleo ya kazi.

Amesema Tanesco itakuwa inatoa ratiba kwa wateja wake ili kutambua ratiba nzima ya upatikanaji wa umeme.

Pia, amewahimiza wananchi kufuatilia ratiba rasmi zitakazotolewa kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii ya shirika hilo na njia nyingine za mawasiliano ili waweze kupanga shughuli zao mapema.

Amewataka wananchi kutokuwa na taharuki, kwa kuwa usumbufu huo ni wa muda na unalenga kukamilisha mradi wa kimkakati utakaoboresha huduma ya umeme nchini.

Amesema wataalamu wake walikaa na kuhakikisha hakuna athari yeyote itakayojitokeza kwa upande wa reli ya treni ya kisasa (SGR).