Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upatikanaji wa haki watajwa kuwa kikwazo Tanzania

Abdalah Katunzi kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari (SJMC) ya Chuo Kikuu vya Dar es Salaam, akitoa mada katika warsha ya Kikao kazi kilichoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Cherr'ys mkoani Morogoro

Muktasari:

Pamoja na maboresho yaliyopo katika mfumo wa utoaji wa haki na ukuzaji na ulinzi wa haki za binadamu nchini Tanzania, ufikiwaji na upatikanaji wa haki limekuwa suala tete.

Morogoro. Pamoja na maboresho yaliyopo katika mfumo wa utoaji wa haki na ukuzaji na ulinzi wa haki za binadamu nchini Tanzania, ufikiwaji na upatikanaji wa haki limekuwa suala tete.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai  8, 2019 na Ofisa Uchunguzi mkuu wa Idara ya Elimu kwa Umma, mafunzo, Utafiti na Nyaraka, Phillip Sungu,  mjini Morogoro katika kikao kazi cha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora kinachofanyika kwa siku tatu.

Sungu amesema waathirika wakubwa katika nyanja hiyo ni watoto na wanawake, hali inayoonyesha kuwa bado kunahitajika maboresho zaidi.

Amesema ni ukweli usiopingika sheria na sera zipo, lakini utekelezaji wa wajibu wa nchi wa mkataba mbalimbali ya kimataifa ya Haki za Binadamu, unakabiliwa na changamoto nyingi.

"Wananchi, hususan wanawake, watoto na watu wenye ulemavu wana fursa ndogo mno ya kuvifikia vyombo vya utoaji haki kutokana na sababu mbalimbali," amesema Sungu.

Amesema miongoni mwa sababu ni pamoja na mifumo iliyopo, kushindwa kumudu gharama, uhaba wa misaada ya kisheria, elimu na uelewa mdogo wa masuala ya sheria na haki za Binadamu miongoni mwa umma na wasimamizi wa utekelezaji wa sheria.

Ametaja sababu nyingine ni upungufu katika utawala wa sheria, hususan utendaji ndani ya sekta ya sheria unaoathiriwa na kurudishwa nyuma na rushwa na miundombinu isiyotosheleza, kutaja bali kwa uchache.

Amesema kwa kutambua hilo, Tume, Wizara ya Sheria na Katiba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Asasi za kiraia, vyombo vya habari kwa kushirikiana na UNDP, kuchukua hatua mbalimbali zitakazosaidia kukuza na kulinda haki za binadamu na ufikiwaji na upatikanaji wa haki kwa watu wote.