Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Umri wamnusuru na kifungo cha maisha jela

Muktasari:

  • Miongoni mwa sababu 10 za rufaa walizowasilisha warufani hao wawili ni pamoja na Dickson Raymond, kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la ulawiti akiwa na umri chini ya miaka 18.
no

Arusha. Mahakama ya rufani imetengua hukumu ya kifungo cha maisha jela aliyohukumiwa Dickson Raymond, baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka minne na nusu, kisha ikabainika Mahakama ilikosea kisheria kumtia hatiani akiwa na umri chini ya miaka 18.

Aidha, Mahakama hiyo imebariki adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa mwenzake, Sadamu Hamisi waliyekuwa wamehukumiwa naye, baada ya sababu zake za rufaa ikiwemo kutotambuliwa kutupiliwa mbali na Mahakama hiyo.

Rufaa hiyo ya jinai ilitokana na uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ulitolewa Juni 6, 2022 ambapo katika kesi ya msingi warufani hao walishtakiwa na kutiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hukumu hiyo imetolewa Mei 8, 2025 na jopo la majaji watatu walioketi Arusha ambao ni Ferdinand Wambali, Panterine Kente na Zainab Muruke na nakala yake kuwekwa kwenye mtandao wa Mahakama.

Awali, mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Dickson na Sadamu walishtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto huyo, Novemba 25, 2018.

Baada ya kusikilizwa kesi hiyo ya msingi, warufani hao walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela ambapo walikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambayo ilibariki hukumu hiyo.

Baada ya kupitia sababu za rufaa za warufani hao na kusikiliza hoja za mjibu rufaa, Mahakama ilimuachia huru Jackson kwani alihukumiwa kinyume na sheria kutokana na umri wake kuwa chini ya miaka 18, huku wakitupilia sababu zingine za rufaa na kubariki adhabu dhidi ya Sadamu.


Ilivyokuwa

Akitoa ushahidi mahakamani hapo, mwathirika wa tukio hilo ambaye alikuwa shahidi wa kwanza wa mashitaka (PW1), alieleza kuwa  warufani hao walimpeleka nyumbani kwa mrufani wa kwanza (Dickson), ambapo walimlaza kitandani na kumvua nguo kisha wakamlawiti kwa zamu ambapo alianza Dickson.

PW1 aliieleza Mahakama kuwa anakumbuka uchungu aliokuwa nao kutokana na kitendo cha unyanyasaji wa kingono na baada ya kumaliza kutenda kosa hilo, walifungua mlango na kumwambia aende nyumbani.

Baadaye siku hiyohiyo, kaka wa mwathiriwa alimuona akijisaidia haja kubwa na alipomuuliza alieleza alichofanyiwa kisha wakamjulisha mama yao (PW2) na tukio hilo kuripotiwa kituo cha Polisi.

Alieleza baada ya kupewa fomu ya Polisi Namba 3 (kielelezo cha kwanza), walimpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mt. Meru kwa uchunguzi ambapo PW3 ambaye ni daktari aliyemchunguza alieleza sehemu ya haja kubwa ya mwathiriwa ilikuwa wazi na imelegea ikiashiria kitu butu kiliingia.

Katika utetezi wao, ambao ulikuwa mfupi sana, wote wawili walijitenga na kosa waliloshtakiwa, hata hivyo mwisho wa kesi hiyo walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.


Rufaa

Kutokana na kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama hiyo, walikata rufaa katika Mahakama Kuu (iliyoketi Arusha) katika Rufaa ya Jinai bila mafanikio.

Katika rufaa ya pili, Mahakama ya Rufani, walikuwa na sababu 10 ikiwemo kuikosoa Mahakama ya kwanza ya Rufaa, kushindwa hukumu iliyotolewa kwa mrufani wa kwanza kwani kwa mujibu wake, hukumu hiyo ni kinyume na kifungu cha 160B cha Kanuni ya Adhabu.

Hiyo ni kwa sababu mlalamikaji wa kwanza alikuwa chini ya umri wa miaka 18 wakati wa kutekelezwa kwa kosa hilo.

Sababu ya pili ni ushahidi wa PW1 kupokelewa ukiwa umekiuka kifungu cha 127 (2) cha Sheria ya Ushahidi, tatu ikiwa ni kucheleweshwa kufikishwa mahakamani, Mahakama ya kwanza ya Rufaa ilipaswa kuona kuwa mahakama hiyo ilikiuka kifungu cha 9(3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Nyingine ni mrufani wa pili hakutambuliwa ipasavyo pamoja na kesi dhidi yao kutothibitishwa bila kuacha shaka pamoja na utetezi wao kutopewa uzito.

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, warufani hawakuwa na uwakilishi wa wakili huku mjibu rufaa hiyo akiwakilishwa na mawakili wa Serikali waandamizi, Eliainenyi Njiro na Neema Mbwana ambao walipinga rufaa hiyo.

Akijibu hoja ya kwanza ya rufaa hiyo, Wakili Neema aliieleza Mahakama kuwa ni kweli kama ilivyo kwa mrufani wa kwanza, maelezo ya kibinafsi yaliyomo katika shitaka hilo alikuwa na umri chini ya miaka 18 wakati anatenda kosa hilo.

Hivyo alisema kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 160(B) cha Kanuni ya Adhabu, mrufani wa kwanza alitiwa hatiani kwa kosa lililopangwa lakini alihukumiwa kifungo cha maisha jela ambacho ni kinyume cha sheria, na kuomba Mahakama wabadilishe na iwe adhabu ya viboko.


Uamuzi majaji

Jaji Kente amesema ikiwa hiyo ni Mahakama ya pili ya rufaa, wajibu wao ni  kutoingilia matokeo ya mahakama ya chini isipokuwa kama kuna uthibitisho wa upotovu wa ushahidi wa kisheria au ukiukaji wa haki.

Amesema wanatathmini upya ushahidi, ambapo wameanza kwa sababu ya pili ya rufaa  na kusema katika makosa yanayohusiana na ngono, isipokuwa katika hali nadra sana, ushahidi wa kweli wa kosa linalodaiwa unatarajiwa kutoka kwa mwathirika.

Jaji Kente amesema swali linalojitokeza ni iwapo  ushahidi wa PW1 ulipokelewa kwa mujibu wa kifungu cha 127 (2) cha Sheria ya Ushahidi, kinachosema kwamba:

"Mtoto mwenye umri mdogo anaweza kutoa ushahidi bila kula kiapo au kuthibitisha lakini, kabla ya kutoa ushahidi ataahidi kuiambia Mahakama ukweli na kutosema uongo wowote."

Amesema katika suala hilo wanaona hitaji hilo halikutimizwa hivyo kiliathiri sana ubora na uaminifu wa ushahidi huo na kuwa badala ya kutupilia mbali ushahidi wa PW1 wanaendelea kutathmini kwa nia ya kuamua uaminifu wake kama inavyotakiwa na sheria.

“Msimamo wa sheria ni kwamba, uwezo wa shahidi kumtaja mtuhumiwa mapema kabisa baada ya kutenda kosa, ni uhakikisho muhimu wa kuaminika,”

“Na ushahidi kwenye rekodi ambayo inaonyesha kwamba mwathirika aliwataja waliomdhulumu mapema, tunaona kuwa alikuwa shahidi wa kuaminika hivyo tunaendelea kutupilia mbali malalamiko dhidi ya uaminifu wake,”amesema.

Kuhusu madai ya mrufani wa pili kutotambulika ipasavyo na kwamba katika mazingira ya kesi hii, ilikuwa ni lazima kufanya gwaride la utambulisho ili kuondoa shaka, jaji alisema inapaswa kukumbuka kuwa PW1 alikuwa amemtaja mrufani wa pili kuwa ni Sadamu au Fundi.

“Pia tunaona kutokana na ushahidi huo mwathiriwa alikuwa akifahamiana naye, tumejiridhisha kuwa mrufani wa pili hakuwa mgeni kwa mashahidi wanaomtambulisha akiwemo mwathirika,” amesema.

Kuhusu kesi kutothibitishwa bila kuacha shaka, Jaji Kente amesema ni sheria iliyoamuliwa kwamba, katika kesi za jinai hukumu lazima inatokana na ushahidi unaoaminika na wa kutosha.

Jaji Kente amesema katika kesi ya Selemani Makumba dhidi ya Jamhuri (supra) ambayo kwa sasa ndiyo mamlaka inayoongoza kwa ushahidi unaohitajika kuthibitisha madai ya kosa la ngono, walishikilia kwamba, ushahidi wa kweli wa madai ya ngono lazima utoke kwa mwathirika.

“Ushahidi wa PW1 ulikuwa kwa kifupi ila kwa kuzingatia ushahidi wa PW3 aliyemchunguza, tunaridhika kwamba ushahidi wake ulithibitisha kwamba mishipa ya haja kubwa ya mwathirika ulikuwa wazi na umelegea kuashiria kupenya kitu butu, “amesema.

Jaji huyo amesema kutokana na hayo yaliyotangulia, hatuna shaka kwamba ushahidi uliotolewa na PW1 ulitekeleza wajibu wa upande wa mashitaka kuthibitisha kosa na wanatupilia mbali sababu hiyo ya rufaa.

Kuhusu sababu ya kwanza, ambapo Dickson anapinga uamuzi wa Mahakama ya kwanza ya rufaa kwa kuendeleza adhabu ya kifungo cha maisha jela wakati alikuwa chini ya umri wa miaka 18 wakati anatenda kosa hilo, wataangalia kama ilitolewa kinyume cha sheria.

Amesema wanaona kwamba hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa mrufani wa kwanza iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi na kuidhinishwa na Mahakama ya kwanza ya rufaa ilikuwa kali hivyo wanakubali sababu hiyo.

“Hukumu ya mrufani wa pili vinathibitishwa na baada ya kuzingatia ukweli kwamba mrufani wa kwanza amekuwa gerezani tangu Desemba 11, 2020 akitumikia kifungo kisicho halali, tunakataa kutoa adhabu ya viboko dhidi yake na kuamuru aachiliwe,” amehitimisha Jaji Kente.